Zikiwa zimebakia takribani wiki 2 kabla ya klabu yake haijapambana na Arsenal aktika mchezo wa hatua ya mtoano ya michuano ya ligi ya mabingwa wa ulaya, kiungo mshambuliaji wa Bayern Munich Thomas Muller amesema Arsenal wanacheza soka safi la kuvutia na kusema timu yao inaelekea katika mchezo dhidi ya Arsenal wakijua haitokuwa kazi rahisi kuifunga timu hiyo ya Arsene Wenger.
Arsenal, ambayo walimaliza nafasi ya pili nyuma ya Dortmund katika hatua ya makundi, watawakaribisha mabingwa watetezi Bayern katika mchezo wa kwanza wa hatua ya mtoano katika dimba la Emirates mnamo February 19.
Na wakati Muller akiamini vijana wa Wenger wataleta upinzani mkubwa kwa Bayern, mjerumani huyo pia anaamini utawala wa Bayern katika soka la ulaya hivi karibuni unaipa nafasi timu yao.
“The Gunners wanacheza soka zuri sana, ndio timu ngumu tuliyopangiwa nayo,; Muller aliiambia Kicker.
“Tuna ubora sawa na timu hii kubwa kutoka kwenye premier league.”
No comments:
Post a Comment