Tuesday 27 May 2014

MAJI YA MAAJABU YANAPONYA, WENYE UKIMWI NA MAGONJWA SUGU WASHANGILIA

Watu mbalimbali wenye magonjwa  wakimiminika kwenye maji ya bwawa nchini Nigeria na kuoga  wakiwa na imani ya kuponywa magonjwa yao.
WANADAMU wanazidi kuegemea kwenye imani utata! Hivi karibuni, watu mbalimbali wenye magonjwa wamekuwa wakimiminika nchini Nigeria na kuoga maji ya bwawa yanayodaiwa yanaponya magonjwa papo hapo.
Watu hao wakiwemo wazee, vijana waume kwa wake na wenye magonjwa mbalimbali wamekuwa wakizama kwenye maji hayo kwa urefu wa futi tatu hadi nne, wengi wakiwa uchi au nguo za ndani tu.
Wengine huchota maji hayo na kuosha sehemu yenye tatizo hasa wale wenye kushindwa kuona au wenye vidonda sugu kama vile kansa, Ukimwi nakadhalika.
Bwawa hilo limepewa jina la Orimiri lipo umbali wa kilomita 3 kutoka mji wa Nachi, Enugu nchini humo na liligunduliwa na watu wa Kabila la Fulani.
Umati wa watu ukizidi kujitosa kwenye maji hayo huku wengi wao wakiwa utupu.
Tangu kugunduliwa kwa bwawa hilo, zaidi ya watu 3000 wameshafika kuyaoga maji hayo kuanzia asubuhi hadi saa 12 jioni.
Hata hivyo, hakuna taarifa za moja kwa moja na uwazi kwamba watu wamepokea uponyaji.
Nigeria ni nchi yenye matukio mengi ya kiimani licha ya mambo ya kisiasa ambapo mpaka sasa wananchi wake wamekuwa wakikumbana nayo.
Wananchi wakiwa wamejaa bwawani kama kwa Babu wa Samunge.
Baadhi ya viongozi wa dini wamekuwa wakiwaambia waumini wao kuamini zaidi katika uponyaji wa Mungu.
Nchini Tanzania, miaka ya karibuni aliibuka Mchungaji Ambilikile Masapile ‘Babu wa Samunge’ akidai ana maji ambayo mtu mgonjwa akinywa anapata uponyaji.
Watanzania wengi, wakiwemo viongozi wa serikali walimiminika kwenye Kijiji cha Samunge, Loliondo kunywa kikombe chenye maji hayo lakini baadaye ilikuja kubainika kwamba, hakukuwa na uponyaji wowote zaidi ya kumwachia babu huyo utajiri.

NDEGE YAANGUKA


Happened today at Mahale Mountains National Park, Kigoma, Tanzania. No casualties. Thank GOD

Baada ya Adam Kuambiana, bongo movie imepata msiba mwingine wa huyu mwigizaji

Screen Shot 2014-05-27 at 8.56.46 AM
Tukiwa na wiki moja toka tumzike muongozaji na muigizaji Adam Kuambiana leo asubuhi imetoka taarifa nyingine ya kifo cha miongoni mwa waigizaji wa kike toka Bongo Movie.
Aliefariki ni mwigizaji anaitwa Rachel Haule ambaye kacheza movie mbalimbali ikiwemo Vanesa in Dilema.
Screen Shot 2014-05-27 at 8.56.59 AM
Chanzo cha kifo chake chake bado hakijafahamika ingawa taarifa za mwanzo zinasema alikua mjamzito na alikwenda Muhimbili kwa ajili ya kujifungua baadae alifanikiwa kujifungua lakini kwa bahati mbaya mtoto alifariki nae hali ilibadilika akapelekwa ICU lakini baadae akafariki.
Hii ni status yake ya mwisho Facebook.
Screen Shot 2014-05-27 at 8.56.22 AM
Moja ya waigizaji walioandika kuhusu kifo cha Rachel ni Shilole >>> ‘sitaki kumkufuru Mugu wangu ila kazi yake haina makosa, tulimpenda ila mwenyenzi Mungu kampenda zaidi, duh.. inauma sana pole Saguda kwa mtihani uliokupata ila tupo pamoja kwa kipindi hiki kigumu

Unajua ni wanajeshi na polisi wangapi wamepangwa kwa ajili ya kombe la dunia Brazil?

brazuka
Mawaziri wa ulinzi nchini Brazil wameweka wazi kuwa zaidi ya vikosi vya kijeshi laki moja na nusu (150,000) vitasambazwa nchini humo kuhakikisha kunakuwa na usalama wa kutosha wakati mashindano ya mwaka huu ya kombe la dunia.
Kwa mara ya kwanza mpira unarejea katika ardhi yake ya nyumbani kwa zaidi ya miaka 60 wakati Brazil ikiwa katika maandalizi ya mwisho ya kuwa mwenyeji wa michuano hiyo mikubwa zaidi duniani ambapo kwa kiasi fulani hali ya usalama imeonekana kuwa si nzuri kufuatia maandamano ya hapa na pale.
brazuka2

Kumekuwa na maandamano ya wananchi wenye hasira wasiotaka mashindano hayo yafanyike, wengi wamekuwa na hasira juu ya kiasi cha pesa kilichotumika kwa ajili ya maandalizi yake zaidi katika kipindi ambacho nchi inakabiliwa na mtikisiko wa kiuchum

Hiki ndio kiwanda kikubwa cha magari kilichofungwa India, madeni yatajwa kuwa sababu.

Ambassador2

Kampuni kubwa ya utengenezaji wa magari aina ya Ambassador ya nchini India imefunga huduma zake za uzalishaji kwa madai ya kugubikwa na madeni na kukosekana na mahitaji ya ya gari hilo ambalo liliuzwa sana na kuweka matabaka katika nchi hiyo kutokana na gharama zake.
Kiwanda hicho cha Hindustan ambacho ni cha zamani zaidi kuliko vyote nchini humo imefunga huduma zake katika Jimbo la Uttarpara Magharibi mwa Bengal ambako imekuwa ikitengeneza magari ya aina hiyo tangu mwaka 1957.
Ambassador car, India

Afisa mkuu wa kiwanda hicho amesema kuwa kazi katika katika kiwanda hicho zimesitishwa na wamefanya hivyo kuhakikisha kiwanda hicho hakitumii fedha zaidi na kuwafanya kuweka mipango mipya ya kukirudisha.

Ushahidi wa T.I juu ya usaliti uliofanywa na mkewe na bondia Mayweather.

TI...

Tayari tumeona bondia Mayweather akitoa ushahidi wake kufuatia ugomvi mkubwa ulioibuka kati yake ya Rapa T.I juu ya usaliti na mke wake Tameka au Tiny na kusema Tiny ndie aliyesababisha kila kitu  ambapo wapenzi hao hawakujibu chochote lakini sasa wameamua kuvunja ukimya kila mtu kwa wakati wake.
Kupitia Instagram, Tiny alianza kwa kuwashukuru mashabiki wake waliosimama pamoja nae na kuwaponda waliokuwa wakimsema lakini akafunguka kuwa mara nyingi mpenzi wake amekuwa akionekana na wasichana wengine lakini yeye alinyamaza tu hakusema chochote iweje watu wahoji baada ya yeye kuonekana na Mayweather?
TI-x-Tiny

Baada ya kukaa kimya kwa muda, Rapa T.I nae akaamua kujibu kupitia Instagram kuwa alijua ishu nzima baada ya kuambiwa kila kitu na kusema hajali tena lakini pia alionyesha kupitia video mkono wake akiashiria kwamba kweli aliingia katika ugomvi na mtu.

Monday 19 May 2014

Taarifa rasmi ya kustaafu soka kwa Ryan Giggs hii hapa

1966912_730304170366864_4292087558580139743_n
Muda mchache baada ya kutangazwa kuwa kocha msaidizi wa klabu ya Manchester United, mwanasoka Ryan Giggs ametangaza rasmi kustaafu soka.
Giggs ambaye alianza kuichezea timu ya watoto ya Manchester United mnamo mwaka 1991, amestaafu soka baada ya kuitumikia klabu hiyo kwa miaka 23 mpaka sasa huku akifanikiwa kuwa mchezaji aliyecheza mechi nyingi zaidi katika klabu yake ya Manchester United – akiichezea mara 963.
Giggs anastaafu akiwa ndio mwanasoka ambaye kashinda makombe mengi zaidi – makombe 13 ya premier league, FA Cup 4, Capital One 4, mawili ya kombe la klabu bingwa ya ulaya na 2 klabu bingwa ya dunia. 

Giggs pia ameshinda tuzo ya mchezaji bora chipukizi wa ligi mara mbili mwaka 1992 na 1993, pia alishinda tuzo hiyo kutoka kwa klabu ya Manchester United mwaka 1991 na 1992. 

Mnamo mwaka 2009 alishinda tuzo ya BBC Sports Personality of the Year na paia akashinda PFA Player of the Year award. Ametajwa kuwa mchezaji bora mwaka wa ligi kwa mara 6.

Huyu Ndiye kocha mpya aliyetangazwa na Man United

u
Klabu ya Manchester United imemtangaza kocha Louis Van Gaal kuwa ndiye Meneja na kocha mpya wa timu kwa msimu ujao,hatua hiyo inakuja wiki kadhaa baada ya klabu hiyo kumtimua David Moyes.
Sababu kubwa ya kutimuliwa kwa Moyes ni kutokana na mfululizo wa matokeo mabaya ya timu hiyo kwa msimu uliopita,Louis Van Gaal ambaye ni kocha wa zaman wa timu za Ajax,Bayern na Fc Barcelona na kawa sasa anaifundisha timu ya taifa ya Uholanzi.
Anategemewa kujiunga na Manchester United mara baada ya kushiriki kwenye michuano ya kombe la dunia ingawa kwa sasa Louis Van Gaal amesaini mkataba wa miaka 3 na amemteua Ryan Giggs kuwa kocha msaidizi.

KUTANA NA RAIS ANAECHEZA MPIRA WA KULIPWA

prezdaa
Nikikupa nafasi ya kuniambia namba ngapi atakua anacheza huyu president wan chi kwenye hili soka unaweza kuotea ni namba ngapi?tunaweka kwenye story kubwa kutokana na kutotokea mara kwa mara kwa taarifa hizi.
prezzz
Sasa unaambiwa Klabu moja huko Bolivia (Sport Boys) imemsajili rais wa Bolivia Evo Morales kucheza kama kiungo wa kati kuanzia Agosti mwaka huu na mgongoni atakua na jezi namba 10.
Mshahara wa Rais Morales kwenye timu hii atakua akilipwa dola $213 kwa mwezi ambapo ni zaidi ya laki 3 kwa pesa za Kitanzania ,klabu hiyo ipo Kusini mwa Bolivia katika jimbo la Santa Cruz.
prez
Kwa sasa Mashabiki wanamsubiri president huyo mwenye umri wa miaka 54 ambaye ni shabiki mzuri wa michezo kucheza mpira.ataichezea Sports Boys, timu iliyopo kusini mashariki mwa mkoa wa Santa Cruz.
Timu hiyo ambayo ipo katika ligi ndogo imesema kuwa rais huyo atakuwa akicheza kwa dakika 20 katika kila mchuano watakaokuwa wanacheza,hasa ikizingatiwa kuwa ni mtu mwenye shughuli nyingi.
Rais Morales amewahi kucheza katika mechi nyingi iliyotambulika pamoja na wanahabari, viongozi wa umoja na marais wengine.
Kumbukumbu inaonyesha mwaka wa 2007 rais huyo alishiriki katika mechi iliyokusudiwa kupinga kikwazo kilichokuwa kimewekewa Bolivia cha kutoshiriki katika mechi za kimataifa katika sehemu zenye urefu.
Ingawa Mwaka wa 2006 alipata matatizo uwanjani kwa kuvunjika mguu wakati alipogongana na kipa

UNAZIKUMBUKA ZILE CHUMA TANO ZA FEO ZIMEANZA KUTEMBEA 2 NA HAWA NDIO MADEREVA WALIOPEWA GARI MPYA.PENDEKEZA JINA LA MADEREVA WATATU UNAOWAFAHAMU WALIOPO KWENYE KAMPUNI YETU ILI WAPEWE GARI MPYA ZILIZOSALIA

KADO BOY AKA BABA KID MWANZO ALIKUA AKIENDESHA T 874 BUY SASA HIVI AMEPEWA T 551 CVR NI MOJA KATI YA MADEREVA WAKONGWE SUPER FEO HAPA AKIWA KATIKA BASI LAKE JIPYA 

NICO MESHACK TOKA T 376 CAX SASA UTAKUTANA NAE KWENYE T 587 CVR HAPA AKIWA KATIKA BASI LAKE JIPYA TAYARI KWA SAFARI

Unaambiwa huyu ndiye nabii wa Tanzania anayeponya ugonjwa wa Dengue kwa Juice.

zabibu
Baada ya time ya Babu wa Loliondo kuponya kwa kutumia kikombe,sasa ni time ya  kiongozi wa dini ambaye anajiita nabii na kutangaza kuwa anatibu ugonjwa wa Dengue kwa kutumia juisi.
Nabii huyu anayejulikana kwa jina la Yaspi Bendera baada ya taarifa zake kusambaa kumefanya baadhi ya wagonjwa kuanza kwenda kwenye kanisa lake la Ufunuo kwa Watu Wote lililopo Yombo Buza-Kipera.
Ingawa Serikali imeonya vitendo vya baadhi ya watu kuwaondoa wagonjwa hospitalini na kuwapeleka kwenye maombi na kusema mtu yeyote anayesababisha wagonjwa kuondolewa hospitalini kwenda kufanyiwa maombi atachukuliwa kuwa ni adui namba moja,katika jitihada za kupambana na ugonjwa huo na kusisitiza kuwa wagonjwa ni lazima kwanza watimize dozi wanazopewa na wataalamu hospitalini ndipo waendelee na imani zao.
Taarifa ya wataalam inasema kuwa ugonjwa huo unatokana na mbu aina ya aedes egypti sasa Nabii Yaspi anadai kuwa homa ya dengue ni pigo lililoletwa na Mungu kwa watu wasiotaka kumtii.
Nabii huyo anadai kuwa alionyeshwa na Mungu miezi miwili iliyopita kuwa homa ya ugonjwa huo ingeibuka nchini na kwamba itawaathiri zaidi watu wazima kuliko watoto.
Nambii huyo kasema kuwa moyoni ana siri nzito ambayo atamwambia mkuu wa nchi peke yake ambaye ni Rais Jakaya Kikwete na endapo atakosa nafasi ya kufanya hivyo hatamwambia mtu mwingine