Sunday 21 September 2014

Boko Haram lashambulia Nigeria Kazkazini

 
 
                                                                Wapiganaji wa Boko Haram

Wapiganaji wa kundi la Boko Haram nchini Nigeria wameshambulia mji wa kazkazini mashariki wa Mainok karibu na mji wa Maiduguri.
Takriban watu thelathini wameripotiwa kufariki siku ya ijumaa wakati wapiganaji hao walipotekeleza mashambulizi katika soko moja lililojaa watu wakati wa mchana.
Walioshuhudia wanasema kuwa wapiganaji hao walibeba chakula katika magari ya wizi,huku wanajeshi wakitoroka.
Kundi la Boko haram limechukua udhibiti wa miji kadhaa na vijiji katika mji wa Maiduguri katika majuma ya hivi karibuni.
Jeshi limejaribu kulikabili kundi hilo licha ya tangazo la hali ya hatari katika majimbo mjatatu ya kazkazini mashariki mwa Nigeria mwaka uliopita

Afghanistan yabuni serikali ya umoja

  
                                               John Kerry,Ashraf Ghani na Abdullah Abdulla

Makubaliano ya kubuni serikali ya umoja wa kitaifa nchini Afghanistan hatimaye yametiwa sahihi ,baada ya miezi kadhaa ya mgogoro kuhusu matokeo ya uchaguzi wa urais mnamo mwezi April na Juni.
Katika makubaliano hayo ya kugawana mamlaka Ashraf Ghani ndio rais mpya huku mpinzani wake Abdullah Abdullah akimchagua afisa mkuu atakayekuwa na mamlaka kama yale ya waziri mkuu.
Ashraf Ghani atakuwa rais mpya mwenye mamlaka mengi na makubaliano hayo yanasema kuwa afisa mkuu atakayechaguliwa atakuwa akiwajibika kwake.
Hatahivyo bwana Ghani amepoteza harakati za kutaka kutawazwa baada ya matokeo ya uchaguzi.
Wawili hao wametia sahihi makubaliano ya kubuni serikali ya kitaifa kabla ya matokeo hayo ya uchaguzi kutangazwa.
Na afisa mkuu atakayechaguliwa na Abdulla Abdullla atakuwa sako kwa bako na rais wakati atakapotawazwa.
Bwana Abdullah alikabidhiwa uwezo wa kuwateua maafisa wengine wa ngazi za juu dhidi ya Ghani.
Makubaliano hayo yanasema kuwa makundi hayo mawili yatashirikishwa vilivyo katika uongozi wa taifa hilo.
Hatahivyo hakutakuwa na usawa wa kuwateua maafisa zaidi katika ngazi za chini za serikali swala ambalo huenda likazua ubishi mkubwa.
Lakini baada ya mgogoro mkubwa wa kampeni za uchaguzi wa miezi kadhaa,udhabiti wa taifa hilo haujulikani.

Ebola:Raia wa Sierra.L waheshimu agizo

 
 Raia wa Sierra Leone wamesalia majumbani mwao kwa siku ya pili mfululizo wakati ambapo taifa hilo linatekeleza agizo la kutotoka nje la masaa 72 ili kujaribu kusitisha ueneaji wa ugonjwa wa Ebola.
Mwandishi wa BBC katika mji mkuu wa Freetown anasema kuwa barabara nyingi za miji ambazo zimekuwa zikijaa watu hazina watu kwa sasa.
Mwandishi wetu anasema kuwa kituo cha oparesheni za dharura kilipokea zaidi ya simu 900 katika siku ya kwanza ya agizo hilo,kupitia kuwaripoti wagonjwa ama kutaka miili ya wafu kuchukuliwa.
Amesema kuwa kuna vituo viwili pekee katika taifa hilo na kwamba kituo kimoja katika eneo la Kenema kimejaa wagonjwa.

MWENYEKITI WA CHADEMA MBEYA VIJIJINI AHAMIA ACT



.
 Asema mizengwe imemuondoa na kwamba hakuna demokrasia ndani ya chama hicho, huku akisema kuwa mengine hayasemeki

Chukua muda wako kupitia kila kilichoandikwa kwenye kurasa za mbele za magazeti ya leo September 21 / 2014

.

.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.

.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.

.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.