Waziri wa uhamiaji wa Uingereza ajiuzulu 
 *Waziri wa Uhamiaji wa Uingereza, Mark Harper (pichani), amejiuzulu baada 
ya kujulikana kuwa amemuajiri mtu asiyekuwa na kibali cha kubaki nchini.*
*Alieleza kuwa alidanganywa na mwanamke mmoja aliyemuonesha nyaraka za 
bandia, alipomuajiri kusafisha nyumba yake.*
*Bwana Harper alisema kwa sababu alichangia kupitisha bungeni sheria ngumu 
kuhusu uhamiaji, alihisi inambidi kuwajibika zaidi kushinda wengine.*
*Chama cha Conservative kimeahidi kupunguza idadi ya watu wanaohamia 
Uingereza kutoka malaki na kuwa elfu kadha tu.*
*Chanzo: BBC Swahili*
 
 
 
 
          
      
 
  
 
 
 
 
 
 
 
 
 
 
No comments:
Post a Comment