| Rais wa Shirikisho la Soka Tanzania, (TFF) Jamali Malinzi, (katikati) akiongea na wandishi wa habari kuhusu Mpango Maalum wa Kuboresha timu ya Taifa, ‘Taifa Stars’ katika Ofisi za Shirikisho hilo zilizopo katikati ya jiji. Kushoto ni Katibu Mkuu wa Shirikisho hilo, Selestine Mwesigwa na kulia ni Rais wa Chama cha Soka Zanzibar (ZDF), Ravia Idarous. | 
SHIRIKISHO
 la Soka Tanzania (TFF) limeanza mikakati ya kuiwezesha timu ya taifa ya
 Tanzania ‘Taifa Stars’ kufuzu kwa Fainali za mataifa ya Afrika (AFCON) 
mwakani baada ya kupanga timu hiyo kuweka kambi nchini Uholanzi.
Kambi
 hiyo maalumu kwa timu hiyo itasaidia kujiandaa na hatua ya kufuzu 
fainali hizo zitakazofanyika mwakani nchini Morocco na kushirikisha 
jumla ya mataifa 16 yatakayofuzu.
Akizungumza
 na jijini Dar es Salaam, Rais wa TFF, Jamal Malinzi amesema endapo 
Stars itafanikiwa kupita katika hatua ya awali ya mchujo ikiwa itapangwa
 kwenye hatua hiyo, wamepanga kuweka kambi nchini Uholanzi ili kujiandaa
 na hatua ya pili ya makundi.
Malinzi
 alisema wameamua kufanya hivyo ili kurudia historia ya mwaka 1979 ya 
Stars kufuzu kwa mara ya mwisho michuano ya AFCON, iliyofanyika nchini 
Nigeria, kwani Stars iliweka kambi Uholanzi kufanikiwa kufuzu kwa 
fainali hizo.
“Tumepokea
 barua ya Shirikisho la Soka Afrika (CAF) inayotueleza kuwa mechi zetu 
za mchujo zitaanza kati ya mwezi Mei hadi Agosti kutokana na kiwango 
chetu kuwa chini ya nchi 21 bora za bara hili, hivyo muda si mrefu 
tunafikiria kurekebisha benchi lote la ufundi kwa pamoja na kuanza 
mikakati ya timu hiyo.
Pia
 alisema wameshazungumza na Balozi wa Uholanzi hapa nchini kwa ajili ya 
mipango yao hiyo, pia wamewataarifu wadhamini wakuu wa Stars, Kampuni ya
 Bia Tanzania (TBL) kupitia kinywaji cha Kilimanjaro Premier Lager ili 
kuandaa bajeti ya ziara hiyo.
 
No comments:
Post a Comment