Kesi ya kuua bila kukusudia inayomkabili msanii wa kike wa filamu Tanzania Elizabeth Michael maarufu kwa jina la
Lulu akituhumiwa kumua msanii mwenzake wa filamu Steven Kanumba imetajwa leo mahakama kuu kanda ya Dar es Salaam.Mnamo
 tarehe 7/4/2012 huko sinza vatican Dar es Salaam mtuhumiwa bila 
makusudi alimua Steven Kanumba.Mshitakiwa na marehemu walikua na 
uhusiano wa penzi.Siku ya tukio mshtakiwa alienda kumtembelea marehemu 
nyumbani kwake sinza akawakuta marehemu na mdogo wake Setty Bosco 
wakijiandaa kutoka saa 12.00pm ya usiku.Ndipo mshtakiwa alifika 
nakuingia ndani kwenye chumba cha marehemu.Mdogo wa marehemu akasikia 
malumbano kati ya Lulu na Kanumba kwa nini anapokea simu za watu 
wengine.Baada ya hapo lulu akataka kutoka nje marehemu akamvuta arudi 
ndani .Baada ya hapo lulu akatoka nje akiwa analia na kumuambia Setty 
Kanumba ameanguka chini.Ndipo Setty Bosco akawasiliana na dokta wake 
kanumba akafika nyumbani na kumfanyia vipimo ikagundulika amefariki 
dunia lakini dokta hakumuambia mdogo ake kanumba mpaka alipopelekwa 
muhimbili ikabainika amefariki dunia kutokana na uvimbe ndani ya 
ubongo.Mshitakiwa alikamatwa Bamaga na kupelekwa kituo cha Polisi cha 
osterbay.Baada ya kusomewa mashitaka hayo mshitakiwa alikana .Upande wa 
jamhuri chini ya wakili mwandamizi Monica
 Mbogo umewasilisha ripoti ya kitabibu na ramani ya tukio pia kutakua na
 mashahidi watano Setty Bosco,Dr Palpas Kageiya,Esther Zefania na E.6056
 Lenatus.Upande wa mshtakiwa wakili Peter Kibatala alisema mashahidi 
wako watano hakuwataja majina.
Hata
 hivyo jaji Rose Temba aliyekua anaisikiliza kesi hiyo amehairisha kesi 
mpaka itakapopangiwa tarehe ya kuanza kusikilizwa rasmi pande zote mbili
 jamhuri na mshitakiwa watajurishwa.
 
No comments:
Post a Comment