Watu
 wawili wanaosadikiwa kuwa ni wezi wameuawa kwa kushambuliwa na wananchi
 waliojichukulia sheria mkononi kwa kisingizio cha kuwa na hasira kali 
katika mtaa wa Mayila kata ya Nyihogo wilayani Kahama Mkoani Shinyanga.
Tukio
 hilo la mauaji limetokea leo majira ya saa tisa alasiri baada ya vijana
 hao kuhisiwa kuhusika na matukio ya wizi ambayo yamekuwa yakitokea 
katika eneo hilo mara kwa mara na kuwakosesha amani wananchi.
Kwa
 mujibu wa Diwani wa Kata ya Nyihogo Amos Sipemba, aliyefika eneo la 
tukio mara baada ya mauwaji hayo, amesema hadi sasa mmoja wa marehemu 
ametambulika kwa jina la Joseph Bakuku huku mwingine akiwa bado 
hajafahamika.
Sipemba
 amesema huenda kufanyika kwa mauaji hayo kunatokana na wananchi hao 
kuwahisi vijana hao kuhusika katika matukio mawili ya uvamizi 
yaliyotokea usiku wa kuamkia jana katika kata hiyo na kuripotiwa ofisini
 kwake.
Jeshi
 la Polisi wilayani Kahama limethibitisha kutokea kwa tukio hilo na 
kwamba miili ya marehemu hao imehifadhiwa katia chumba cha kuhifadhia 
maiti cha hospitali ya Wilaya ya Kahama, huku uchunguzi wa tukio hilo 
ukiendelea.
 
No comments:
Post a Comment