Friday 18 July 2014

DIAMOND ANYEMELEWA NA LAANA YA BABA

Wakati akimpa mama yake, Sanura Kassim ‘Sandra’ gari la Sh. milioni 38 huku akitawanya mamilioni ya fedha kwenye matukio mbalimbali, staa wa Bongo Fleva, Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’ anadaiwa kunyemelewa na laana kufuatia baba yake, Abdul Jumaa kuugua na kuvimba miguu bila msaada wowote.
Staa wa Bongo Fleva, Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’ akila ujana na mpenzi wake Wema Sepetu.

Kwa mujibu wa chanzo makini cha Ijumaa, baba wa staa huyo anayeishi Magomeni-Kagera jijini Dar, amekuwa akisumbuliwa na tatizo la kuvimba miguu na hakuna msaada wowote anaoupata kwani chanzo cha mapato anachokitegemea ni kodi tu ya nyumba ambayo anaipata kutoka kwa wapangaji wachache alionao.
BOFYA HAPA KUKISIKIA CHANZO
“Yaani tunashangaa kusikia Diamond ana fedha nyingi, juzikati tuliona katika gazeti kamnunulia mama yake gari la milioni 38 (Toyota Lexus-Harrier) sasa kwa nini asimthamini baba yake hata kidogo? 
“Ukweli ni kwamba baba Diamond anasumbuliwa na tatizo la miguu kuvimba.

“Amekuwa akilalamika mara kwa mara lakini Diamond hatujawahi kumuona,” kilinyetisha chanzo hicho na kuongeza:“Juzikati hapa baba Diamond alishikika kwelikweli miguu, akaugulia mwenyewe ndani pasipo kuwa na msaada wowote tena nasikia mzee huyo hataki hata kuongelea lolote kuhusu Diamond maana haoni umuhimu wa kufanya hivyo wakati amemsusa muda mrefu sana.”
MATIBABU HAYAZIDI MILIONI
Katika aya nyingine, chanzo hicho kilidai kwamba ugonjwa wa miguu ambao unamsumbua mzazi huyo, gharama za matibabu haziwezi kufikia hata shilingi milioni moja za madafu achilia mbali mamilioni anayoyatapanya staa huyo.

Mama yake Diamond,Sanura Kassim ‘Sandra’ akilitesti gari alilokabiziwa na Mwanaye kama zawadi.

“Ingekuwa tatizo kubwa sana, hapo sawa, kwa sababu miguu huwa inamvimba lakini akipata dawa za kutumia huwa inarudi katika hali ya kawaida, kwa nini lakini anamfanyia hivyo baba yake? Amemkosea nini?” Kilihoji chanzo hicho.
UTAJIRI WAKE WAANIKWA
Wakati chanzo hicho kikiweka nukta hapo kwa muda, mapaparazi wetu walipewa malalamiko mengine kutoka kwa jirani mmoja wa baba Diamond ambaye alimsihi amsaidie mzazi wake kwani anaamini uwezo anao kupitia kumbukumbu ambazo Diamond mwenyewe alizithibitisha kupitia vipindi mbalimbali vya runingani kama Take One na Spora Show vya CloudsTV.

Pia kwenye vyombo vingine vya habari zikiwemo redio na magazeti pendwa ya Global Publishers.
Jirani huyo alidai kwamba mwaka jana Diamond alitangaza kuwa ana utajiri wa Sh. bilioni moja ikiaminika kwamba mwaka huu umeongezeka mara dufu.

“Nakumbuka mwaka jana kupitia Kipindi cha Spora Show na kile cha Take One, Diamond alikiri kuwa ana mkwanja usiopungua bilioni moja, hiyo ilikuwa kwa mwaka jana, sasa mwaka huu unadhani atakuwa na shilingi ngapi? Aache hizo bwana, amsaidie baba yake hata kwa kumpa mtaji mdogo wa biashara ambao unaweza kumsaidia,” alisema jirani huyo.
MATANUZI  YA DIAMOND, WEMA
Katika kuendelea kuichimba habari hiyo, mapaparazi wetu walinasa malalamiko kutoka kwa jirani mwingine wa mzazi huyo ambaye alieleza masikitiko yake kwa kulinganisha starehe ambazo staa huyo anazifanya na asali wake wa moyo, Beautiful Onyinye, Wema Isaac Sepetu na maisha halisi ya baba yake.

“Mimi ni mfuatiliaji mzuri wa habari za mastaa, naona kila siku kwenye vyombo vya habari jinsi gani Wema na Diamond wanavyotumia fedha nyingi katika masuala ambayo hayana ulazima kiivyo.
“Sisi kama majirani hatupendezwi na hali hii, angekuwa anakuja angalau siku mojamoja kumuona baba yake kuliko kila siku kumhudumia mama yake pekee,” alisema jirani huyo.

Baba yake Diamond, Abdul Jumaa akitafakari jambo.

TATIZO NI NINI?
Mapaparazi wetu waliingia mzigoni kusaka kiini halisi kwa nini Diamond amwage fedha nyingi kwa mama yake pasipo kumkumbuka japo kiduchu baba yake ambapo ilielezwa kuwa staa huyo wa Mdogomdogo hakuwa na ugomvi wowote na mzazi wake huyo.

“Kama ni ugomvi ulikuwepo kati ya mama na baba lakini Diamond hahusiki, tunashangaa kuona kama staa huyo naye anaweza kumsusia baba yake,” kilieleza chanzo na kuongeza:
“Mbaya zaidi nasikia Diamond amekuwa mzito kupokea simu za baba yake, sasa huoni kama siyo jambo la busara, mzazi ni mzazi tu hata iweje. Kwa mtazamo wangu kinachofuata ni laana.
“Kuna mifano ya watu wengi ambao waliingia kwenye laana za wazazi wao na wakajikuta kama siyo kufulia kama (wanatajwa mastaa waliofulia wa muziki Bongo) au hata kukutwa na umauti.
“Jambo hili si la kibinadamu tu, kwa wale wanaosoma vitabu vitakatifu watakuwa na mifano mingi ya watu waliowakosea wazazi wao wakalaaniwa.”

BABA DIAMOND ANASIKITISHA
Ijumaa lilipomtafuta baba Diamond kwa njia ya simu aliongea maneno ya kusikitisha huku akikataa katakata kumzungumzia kijana wake huyo.

“Jamani naomba mumuache Diamond na maisha yake, sitaki kabisa kusikia habari zake maana hata nikiongea naonekana najipendekeza kwake.
“Namshukuru Mungu, kama ni kuumwa kwa sasa naendelea vizuri na maisha yangu, niacheni nipumzike,” alisema mzee huyo kwa unyonge.
DIAMOND ANASEMAJE?
Alipotafutwa Diamond ili kumsikia anazungumziaje madai hayo, simu yake iliita bila kupokelewa. Tunaamini atasoma habari hii hivyo si vibaya akatutafuta ili afunguke kwa upande wake.

MAONI YA MHARIRI
Diamond ni staa mkubwa kwa sasa ndani na nje ya Bongo, uwezo alionao kifedha unapaswa kuendana na baraka za wazazi wa pande zote mbili. Vitabu vya Mungu vinatufundisha kwamba wazazi ndiyo Miungu wetu hapa duniani hivyo hata kama kuna kosa amefanya, mzazi atabaki kuwa mzazi tu. Hatutakiwi kumkosoa!

Tuesday 8 July 2014

YA MAKAMBA NA URAIS

 http://www.mwananchi.co.tz/image/view/-/1689972/highRes/460607/-/maxw/600/-/156ucvh/-/makamba.jpg
 
 
Kauli ya Naibu Waziri wa Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia, January Makamba, kwamba, Tanzania inahitaji kiongozi kijana katika nafasi ya urais mwenye fikra mpya katika uchaguzi mkuu ujao, imeelezwa kuchochea mtafaruku ndani ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) mkoani hapa.

Katibu Mwenezi wa Itikadi na Siasa wa (CCM) Wilaya ya Shinyanga Mjini, Charles Shigino, alisema hayo alipozungumza na waandishi wa habari jana.Alisema usemi huo ni kuleta siasa za ubaguzi ndani ya chama. 
Shigino alisema CCM inapiga vita ubaguzi wa aina yoyote ndani ya chama na kuongeza kuwa kauli ya Makamba ni silaha tosha ya kukivuruga chama, hivyo anapaswa kuomba radhi.
 


“Kauli ya Makamba siyo ya kiungwana. Nadhani aliropoka, hakufikiria anachokisema. Na katika nchi hii ndiyo imekuwa ikiongozwa na wazee ndani ya miaka mingi na kuwa katika mstari mnyoofu.

Hivyo, wazee wanapaswa kupewa heshima zao na kijana huwezi kufanya jambo la maana bila ya kuwa na mzee nyuma yako,” alisema.
Aliongeza: “Katika ulimwengu huu wa sayansi na teknolojia siyo kwamba, nchi ndiyo itawaliwe na vijana tena katika nafasi nyeti ya urais. Makamba anatakiwa kujitathmini mara mbili mbili. Wazee ndiyo nguzo ya nchii hii. Wanaifahamu tokea enzi za uhuru. Sisi tumekuta historia tu.”


“Kama kweli Makamba kama ana nia ya urais, ni bora akajipa muda wa kujifunza na kupata uzoefu wa kutosha wa nafasi ya uongozi katika nafasi hiyo. Kwani Watanzania wanajua bila ubishi kuwa katika nafasi ya uongozi ndani ya CCM hana muda wa mwaka mmoja na nusu.”

Alisema kisiasa Makamba bado ni mdogo na kwamba, anatakiwa kwenda kujifunza kutoka kwa wazee waliopo ndani ya CCM, ambao yeye amekuwa akiwadharau.
Shigino alisema Makamba anatakiwa kujua kuwa Watanzania wanapomchangua mgombea urais kupitia CCM ndiye huyo huyo atakayekuwa Mwenyekiti wa CCM Taifa.
Alisema kwa sasa taifa lilipofikia linatakiwa kuongozwa na kiongozi mwenye maamuzi ya kutosha pamoja na uzoefu wa kukabiliana na changamoto zilizopo, hasa katika nyanja ya uchumi, mendeleo ya jamii pamoja na siasa yenye utawala bora.
 
CHANZO: NIPASHE

MNYIKA ADAI KUTISHIWA



John Mnyika

MBUNGE wa Ubungo, John Mnyika (Chadema), amewaomba wapiga kura wake kumuombea kila siku kutokana na madai kuwa amekuwa akiwindwa na watu wanaotishia uhai wake.
Mnyika alitoa kauli hiyo juzi jioni katika eneo la Mbezi mjini Dar es Salaam, wakati akihutubia mkutano wa hadhara.
“Nimekuwa nikizungumza mambo mengi ninapokuwa bungeni Dodoma, hasa ninapowatetea wananchi na wapiga kura wangu, lakini kuna watu hawafurahishwi kabisa…sasa wamefikia hatua ya kunitishia maisha yangu.
“Wengi mnakumbuka kwamba, Mwenyekiti wa Chama cha Madaktari Tanzania (MAT), Dk. Steven Ulimboka, alitekwa na kupigwa na watu wasiojulikana na kisha kung’olewa meno, baada ya tukio lile aliyekuwa akifuatia nilikuwa mimi, sasa sijui na mimi wanataka kunifanyia hivyo au la,” alisema Mnyika.
Alisema taarifa za yeye kutishiwa maisha zilianza kuvuja baada ya kumalizika kwa vikao vya Bunge la Bajeti.
Alisema kashfa ya Kampuni ya kufua umeme ya IPTL ilianza miaka ya tisini, baada ya maridhiano kati ya Serikali ya Tanzania na Serikali ya Malaysia ili kuleta mitambo ya kufua umeme nchini na kwamba, Rais Jakaya Kikwete anafahamu kiini cha mzozo.
Alisema IPTL imekuwa ikiitia hasara kubwa Serikali kwa kipindi kirefu, jambo ambalo halina budi sasa kuchukuliwa hatua.
“Wenzetu walikuwa na mtaji mdogo walipokuja kiasi ambacho hata Mtanzania anayefanya biashara ndogo ndogo aliweza kuumiliki, lakini uliongezeka kutokana na sisi kupandishiwa gharama za umeme kwa mujibu wa ushahidi wa Mahakama,” alisema

MWENGE WA UHURU WAZUA BALAA WATU SITA WANUSURIKA KIFO

WATU  sita  akiwemo kiongozi wa mbio za mwenge kitaifa Rachel Kasanda wamenusurika  vifo baada ya magari waliokuwa wamepanda kugongana uso kwa uso katika eneo la power station lililopo Namtumbo  Mjini mkoa wa Ruvuma.
 
Akizungumza ofisini kwake kaimu kamanda wa polisi wa mkoa wa Ruvuma George  Chiposi alisema kuwa tukio hilo  limetokea july 8 mwaka huu majira ya saa 12:30 asubuhi  huko katika eneo la power station Namtumbo.
 
Alifafanua zaidi  kuwa inadaiwa  gari lenye namba za usajiri STK 6534 Nissan Patrol ambalo  lilikuwa linaendeshwa na John Dominic Nchimbi (46) mkazi wa songea mjini iligongana uso kwa uso  na gari nyingine  yenye namba za usajiri T 493 ANU Rover4  amabayo ilikuwa ikiendeshwa na Ally  Juma (29) mkazi wa Namtumbo  na kusababisha magari yote mawili kuharibika .
 
Alisema kuwa uharibifu uliotokea  kwenye magari hayo ni kwamba  kila gari liliharibika  lakini watu wote walikuwemo kwenye magari hayo walitoka salama.
 
Alieleza zaidi kuwa  gari lenye namba za usajiri STK 6534 Nissan Patrol  ilikuwa  inatoka kumchukua mkimbiza mwenge kitaifa Rachel kwenye hotel alikokuwa amefikia kwenda eneo la kijiji cha suruti ambako mwenge ulikuwa umelala tayari kwa kuanza safari  ya kwenda wilayani Tunduru.
 
Amewataja abiria waliokuwemo kwenye gari  hiyo aina ya rover4 iliyokuwa ikiendeshwa  na Ally Juma kuwa ni Omary Ngonyani (23) mkazi wa songea, Irene Kitula  (38) mkazi wa Namtumbo, Sekera Mwamwezi  mkazi wa Namtumbo na kwenye gari aina ya Nissan iliyokuwa ikiendeshwa na Nchimbi ilimbeba mkimbiza mwenge kitaifa Rachel .
 
Kaimu kamanda  Chiposi alisema kuwa  dereva wa gari  la rover4 anashikiliwa na polisi kwa mahojiano zaidi na chanzo cha tukio hilo la ajali kinachunguzwa

Sunday 6 July 2014

MASHABIKI WA MBEYA CITY TAWI LA SIDO WAIFANYIA SHEREHE TIMU YAO.

Laizer Ngela Katibu wa Mbeya city tawi la Sido aliesimama akitoa neno la shukrani kwa wachezaji wa Mbeya city
Abubakari Masoli Meneja matukio wa TBL  Mbeya akitambulisha kinywaji cha Grand Malt kwa wachezaji wa Mbeya City
Mwenyekiti wa Timu ya Mbeya City, Musa Mapunda, akizungumza kwa niaba ya Meya wa Jiji la Mbeya, Atanus Kapunga katika sherehe hizo
katibu wa Mbeya City, Emmanuel Kimbe akiongea na mashabiki wa Mbeya city wa tawi la Sido
Mc Lambat
Meneja wa Hotel ya GR  Sam Erick 
MASHABIKI wa Timu ya Mbeya City tawi la Sido jijini Mbeya wameipongeza timu hiyo kwa mafanikio waliyoyapata katika Msimu uliopita wa Ligi kuu Bara uliomalizika kwa timu hiyo kuibuka mshindi wa tatu.
Pongezi hizo zilitolewa jana katika Sherehe iliyoandaliwa na Tawi hilo zilizofanyika katika ukumbi wa Hoteli ya Gr iliyopo Soweto jijini Mbeya na kudhaminiwa na Kampuni ya Bia Tanzania(TBL) iliyohudhuriwa na wachezaji wote wa Mbeya city pamoja na viongozi na mashabiki.
Wakizungumza katika sherehe hizo. Mashabiki hao walisema timu hiyo imeweza kuzitikisa timu kongwe na kubwa hapa nchini hivyo hawana budi kutoa ushirikiano kwa timu yao katika msimu ujao ili iweze kuibuka katika nafasi mbili za juu.
Kwa upande wake Mwenyekiti wa Timu ya Mbeya City, Musa Mapunda, akizungumza kwa niaba ya Meya wa Jiji la Mbeya, Atanus Kapunga, alilipongeza Tawi la Sido kwa kuonesha uzalendo kwa timu yao na kuwa chachu ya mafanikio ya timu.
Alisema mashabiki wa Mbeya city tawi la Sido limekuwa likishiriki shughuli nyingi za timu ikiwa ni pamoja na kusafiri na timu kila timu inapoenda kwa gharama zao wenyewe tofauti na matawi mengine ambayo hutaka kuchangiwa.
Alisema mafanikio ya Mbeya city hayapendwi na watu wengi hususani wapinzani wao hivyo ni vema mashabiki wakaunga mkono kwa nguvu zote ili kuhakikisha timu inafanya vizuri tofauti na wao wanavyotaka.
Aidha katika Sherehe hizo Wachezaji wa Mbeya city walitambulishwa mbele ya mashabiki pamoja na kukabidhiwa zawadi zilizotolewa na Abubakar Masoli,ambaye ni Meneja matukio wa Kampuni ya Bia (TBL) Mbeya.
Naye katibu wa Mbeya City, Emmanuel Kimbe, alisema shughuli zote za kiuchumi za timu hiyo zitashirikisha moja kwa moja mashabiki na matawi pamoja na Halmashauri ili kuhakikisha ushirikiano unadumu kwa mafanikio ya timu.

Degree ya heshima ya udaktari aliyopewa mwanamuziki Oliver Mtukudzi.

MUTU2

Mwanamziki mkongwe wa kimataifa nchini Zimbabwe Oliver Mtukudzi ametunukiwa tuzo ya tatu iliyobeba heshima ya udaktari kutokana na kuwa mshauri na balozi mzuri wa muziki.
Mwaka 2003 alitunukiwa tuzo kubwa ya heshima na chuo kikuu cha Zimbabwe kwa kutambua miongo kadhaa ya mchango wake na kujitolea katika kujenga muziki na msukumo wasanii wa kizazi kipya nchini Zimbabwe huku akionyesha ushawishi kwenye kazi za wasanii hao.
MUTU
Mwaka 2009, Chuo Kikuu cha Wanawake cha Afrika kilimpatia tuzo ya shahada ya sanaa na kumwelezea mwanamuziki huyo kama mbunifu wa hali ya juu kuwahi kutoke nchini Zimbabwe katika kipindi cha miongo mitatu iliyopita.
Oliver Mtukudzi ni mwanamuziki mkongwe kutoka nchini Zimbabwe ambaye amevuma sana na kuvuka mipaka kutokana na nyimbo zake zinazohamasisha amani na kutoa burudani barani Afrika ambapo amekua akitumika kama alama katika taifa hilo haswa kwa upande wa sanaa ya nchini Zimbabwe

Kilichojiri kwenye mechi ya Uholanzi vs Costa Rica – matokeo na wafungaji

20140706-031043-11443153.jpg
Historia mpya imeandikwa kwenye mechi ya mwisho ya hatua ya nane bora iliyozikutanisha Uholanzi dhidi ya timu ya Costa Rica, ambayo kwa mara ya kwanza imefanikiwa kucheza hatua ya robo fainali ya kombe la dunia.
Mchezo huo uliomalizika hivi punde umetumia zaidi ya dakika 120 ili kuamua timu ya kwenda kuchuana na Argentina kwenye nusu fainali.
Dakika 90 za mchezo huo ziliisha kwa matokeo ya sare tasa, na mpaka mpira unakwenda dakika 30 za nyongeza na kumalizika milango bado ikabaki migumu na ikaamuliwa kwenda kwenye mikwaju ya penati.
Uholanzi ikiwa haijawahi kushinda kwenye mikwaju ya penati katika mashindano ya kombe la dunia, ikafanikiwa kushinda kwa penati 4-2 dhidi ya Costa Rica.
Pia hii ni mara ya kwanza kwa Uholanzi kushinda mechi yoyote ambayo imevuka kwenda kwenye hatua ya dakika za nyongeza.
Kwa matokeo hayo sasa Argentina itakutana na Holland jumatano usiku, wakati Brazil ikukutana na Ujerumani jumatatu hii

SIMU ZA MKONONI ZAWASAIDIA WAGONJWA WA KISUKARI SENEGAL

simu

Kwa mara ya kwanza wagonjwa wa kisukari nchini Senegal wameanza kupokea ujumbe wa simu ukiwataka kufunga kwa kipindi cha kabla, wakati na baada ya mwezi wa Ramadhan.
Senegal imekuwa nchi ya kwanza kuanza kutumia huduma hiyo ya simu kuwasaidia wagonjwa kisukari njia muhimu na salama za kuweza kukabiliana na kulinda afya zao haswa katika kipindi hiki cha mfungo.
Wagonjwa walioanza kupokea huduma hiyo wanasema inawasaidia sana.
Marie Gadio, mwenye umri wa miaka 26, ambaye aligundulika kuugua ugonjwa wa kisukari akiwa na miaka 13 anasema kuwa kukabiliana na ugonjwa huo kipindi cha mwezi wa Ramadhan sio kitu rahisi

Hii ndio idadi ya waliokufa baada ya mji wa Lamu Kenya kukumbwa na mashambulizi ya risasi.

lamu

Wizara ya mambo ya ndani Kenya imesema kuwa zaidi ya watu 29 wameuawa katika mashambulizi mawili tofauti katika makazi ya Pwani ya nchi hiyo karibu na mpaka wa Somalia.
Watu 20 waliuawa katika eneo la Gamba kaunti ya Tanariver huku tisa wengine wakipoteza maisha kufuatia mashambulizi ya kufyatuliana risasi katika kituo kimoja cha kibiashara kaunti ya lamu karibu na mpaka wa Somali.
lamu2

Kundi la wapiganaji wa Al shabaab limekiri kutekeleza mashambulizi hayo ambapo inadaiwa watu walikuwa wakiangalia mechi za kombe la dunia wakati wa tukio hilo.
Mashuhuda wanasema watu kadhaa wenye silaha walifika katika kituo cha biashara katika eneo la Hindi jimbo la Lamu, mapema siku ya jumamosi jioni na kuanza kufyatua risasi za moto.
Mashambulizi katika eneo Lamu mapema mwezi uliopita yalisababisha vifo vya watu 60, wakati wanamgambo wa al shaabab wakivamia hoteli na vituo vya polisi.

TAMKO LA BARAZA LA MAOSKOFU TANZANIA

Rais wa Baraza Maaskofu Katoliki Tanzania, Askofu Tarcisius Ngalalekumtwa
Akisisitiza jambo
BARAZA la Maaskofu Katoliki Tanzania limewatoa hofu watanzania katika tamko lake lingine kwa Bunge Maalumu la Katiba (BMK) likisema haliko nyuma ya viongozi wala chama chochote cha siasa kama baadhi yao wanavyofiki.

Akitoa tamko hilo mjini Iringa jana, Rais wa Baraza hilo ambaye pia ni Askofu Mkuu wa Jimbo Kuu la Iringa, Askofu Tarcisius Ngalalekumtwa alisema; “Baraza la Maaskofu Katoliki halina chama katika hili, lakini pia halina mtu au mwanasiasa au chama linachokifanyia kampeni kwa ajili ya Uchaguzi Mkuu wa mwakani.”

Katika Jubilei ya miaka 25 ya uaskofu wa Askofu Ngalalekumtwa iliyofanyika mjini Iringa hivi karibuni, Makamu wa Rais wa Baraza hilo, Askofu Severine Niwemugizi alitoa tamko kuhusu mchakato huo kwa kuwataka Umoja wa Katiba ya Wananchi (Ukawa) kurudi katika bunge hilo bila masharti.

April 16, mwaka huu, wajumbe wanaounda umoja huo, waliamua kutoka nje ya bunge hilo wakipinga kile wanachosema ni kupuuzwa kwa makusudi maoni ya wananchi wanaotaka muungano wa muundo wa serikali tatu kama ilivyopendekezwa katika rasimu hiyo.

Katika tamko hilo Askofu Ngalalekumtwa alisema; “katika ujumbe wetu wa kichungaji wa Pasaka 2014, sisi maaskofu Katoliki Tanzania tuliwaandikia barua watu wote wenye mapenzi mema kwa nchi yetu tukiwaalika kuchukulia maanani mchakato wa kuandika katiba mpya.”

Alisema “wakati huu tunawaalika watanzania wote kwa pamoja, tuungane kuwakumbusha wale waliopewa dhamana ya kukamilisha Rasimu ya Pili ya Katiba kuwajibika binafsi na katika maridhiano kutupatia katiba maridhawa.”

Alisema wajumbe wa bunge hilo wanapasa kujadili kwa umakini kila kilichopo katika rasimu hiyo ili wafikie muafaka utakaoenzi ujasiri wa kipekee wa Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania, Jakaya Kikwete wa kuanzisha mchakato huo.

“Tunawaasa tukiwaombea dhamiri zao zipate maoni mapya ili waweze kubeba kikamilifu dhamana hiyo waliyokabidhiwa,” alisema.

Askofu Ngalalekumtwa alisema baraza la maaskofu katoliki linawataka wajumbe  wa bunge hilo kuwa wamoja na kufanya kazi yao kwa mtazamo usioegemea siasa za vyama.

Alisema ni mategemo yao majadiliano yatafanyika kwa kuheshimiana, kutumia hoja za kizalendo na kiungwana na kuyaangalia kwa mapana mambo na masuala makuu yaliyopendekezwa katika rasimu hiyo.

“Kuandika katiba ni kazi iliyo ngazi ya juu zaidi ya siasa za vyama, na hivyo utashi wa kisiasa wa kuunda katiba mpya kwa kuzingatia Rasimu ya Pili utaweza kuridhiwa kwa kuzingatia msingi huu,” alisema.

Alisema kwa kadri nchi iliyivyo hivisasa kuna sababu za kutosha za kutaka Katiba mpya zikiwa ni pamoja na ufisadi, wananchi kujisikia kukosa usalama na amani, nchi kutokuwa na dira na tunu msingi.

“Na kwahiyo tunawasihi kwa mara nyingine tena ninyi wajumbe wa bunge hilo kurejea katika sehemu ya pili ya mjadala hapo mwezi Agosti mkiwa na moyo na mtazamo mpya,” alisema.

Alisema kwa kazi hiyo wajumbe hao watawasaidia watanzania waendelee kujivunia kuwa na taifa adilifu lenye amani na linalofanya kazi kwa pamoja kwa ajili ya manufaa na ustawi wa wote.

Alisema ikiwa matokeo yatakuwa yenye kuleta mema na kuimarisha amani na utulivu wa nchi, watanzania wote watawashukuru na kuwasifu na kama tunda la kazi ya bunge hilo litakuwa ni lenye kuingiza nchi katika matatizo zaidi, kuwataabisha wananchi na kukosa maelewano baina yao, basi watanzania watawahukumu na kuwawajibisha kwa kukosa umakini katika jukumu hilo muhimu mlilokabidhiwa.

Askofu Ngalalekumtwa alisema nchi haiko tayari kurudi nyuma na kuendelea na maisha yanayoongozwa na Katiba ya 1977 kwahiyo mahitaji ni kuwa na katiba itakayowezesha ushiriki kamili wa watu katika maamuzi na vipaumbele vya maendeleo ya Taifa.

“Tunataka Katiba ambayo inaruhusu utawala wa sheria, haki sawa kwa wote, manufaa na ustawi kwa wote na kuheshimu utu wa kila mmoja. Katiba shirikishi katika matumizi ya madaraka ili yatumike katika kuhudumia wote badala ya wachache na inayoweza kuzuia matumizi mabaya ya madaraka na ufisadi,” alisema.

Alipoulizwa msimamo wake nini kuhusu muundo wa serikali, Askofu Ngalalekumtwa alisema; “siwezi kusema popote pale, naogopa kuwapa ushawishi watu wetu na ndio maana msimamo wa kanisa ni kuwataka wajumbe wote warejee, wajadiliane na kutuletea katiba itakayokuwa na sifa hizo.”

KIJANA MWINGINE AFA JKT


Nimepokea kwa masikitiko makubwa msiba wa Raphael Kingaz aliyekuwa mwanafunzi wa HGE shule ya sekondari mbezi beach, mauti yamemkuta akiwa Tanga kwenye kambi ya mafunzo ya JKT.

Mtoa taarifa wangu wa kuaminika aliyezungumza mtandao huu jamvilahari.com alisema mauti yalimfika jana jioni na mazishi yanatarajia kufanyika kesho. sababu ya kifo chake bado hatujaipata.



Pole ziwafikie ndugu, jamaa na marafiki na jumuiya yote ya shule ya sekondari mbezi beach



HAPA CHINI NI TAARIFA ILIYOTOLEWA NA JKT KUKANUSHA VIFO VINAVYOTOKEA JKT HAVITOKANI NA UKATILI

                                          TANGAZO
JESHI LA KUJENGA TAIFA, LINAKANUSHA TAARIFA ZINAZOSAMBAZWA KWA KUTUMIA UJUMBE MFUPI WA MANENO (SMS) KATIKA SIMU ZA VIGANJANI NA MTANDAO WA JAMIIFORUM.COM, KWAMBA VIJANA WA KUJITOLEA NA MUJIBU WA SHERIA WANAOENDELEA NA MAFUNZO KATIKA MAKAMBI YA JKT WANAKUFA KWA UKATILI, WAKITOLEA MFANO KAMBI YA JKT OLJORO ARUSHA KWAMBA KUNA VIJANA WATATU WAMEFARIKI DUNIA.

UMMA UFAHAMU KUWA TAARIFA HIZO SI ZA KWELI NI UPOTOSHAJI KWA VIJANA NA WATANZANIA. UKWELI NI KWAMBA KUNA KIJANA MMOJA WA KIKE HONORATA VALLENTINE OISO ALIYEFARIKI KATIKA KIKOSI CHA JKT OLJORO ARUSHA KWA UGONJWA WA UPUNGUFU WA DAMU (ANAEMIAULIOSABABISHWA NA MALARIA. SIO VIJANA WATATU KAMA INAVYOELEZWA KWENYE UJUMBE UNAOSAMBAZWA. WAZAZI WA KIJANA ALIYEFARIKI PIA WALITHIBITISHA KUWA KIJANA WAO ALIKUWA NA MATATIZO YA UPUNGUFU WA DAMU.

JESHI LA KUJENGA TAIFA LINASISITIZA KUWA HAKUNA UKATILI WOWOTE UNAOFANYWA KWA VIJANA WANAOENDELEA NA MAFUNZO KATIKA MAKAMBI YA JKT.

JKT LINALAANI KITENDO HICHO NA LINAFUATILIA ILI KUBAINI CHANZO CHAKE. MTU YEYOTE ATAKAYEBAINIKA KUWA NDIYE CHANZO CHA UJUMBE HUO, HATUA ZA KISHERIA ZITACHUKULIWA DHIDI YAKE.

JESHI LA KUJENGA TAIFA LINAWAKUMBUSHA VIJANA NA WATANZANIA KUWA MAKINI NA MATUMIZI MABAYA YA SIMU ZA MIKONONI NA MITANDAO YA JAMII, HASA KWA TAARIFA ZINAZOHUSISHA JESHI.

                                 TANGAZO HILI LIMETOLEWA NA MAKAO MAKUU YA JKT

Saturday 5 July 2014

Hili ndilo Jumba la kifahari Oscar Pistorius alilopanga kuishi na mpenzi wake kabla ya kumuua.

oscar2
Hizi ni baadhi ya picha Jumba kubwa la kifahari la Oscar Pistorius lenye thamani ya Paundi 530,000 ambalo alipanga kuhamia na mpenzi wake Reeva Steenkamp kabla ya tukio la kumpiga risasi akiwa bafuni ambapo kesi yake bado inaendelea.
Pistorius tayari alikwishalipia nyumba hiyo baada ya makubaliano na mpenzi wake huyo baada ya kutembelea nyumba hiyo ambapo wapenzi hao waliwaambia marafiki zao juu ya mpango wa kuhamia katika nyumba hiyo jijini Johannesburg.
oscar1
oscar3
oscar4
oscar5
oscar6
oscar7
oscar8
oscar9

MLIPUKO WATOKEA KARIBU NA BUNGE LA SOMALIA

somalia2
Mlipuko mkubwa umetokea na milio ya risasi imeripotiwa karibu Bunge la Somalia wakati wabunge wakiwa katika kikao chao.
Kwa mujibu wa BBC, Ripoti za awali zinasema kuna watu kadhaa wamejeruhiwa kutokana na mlipuko huo unaosemekana umesababishwa na bomu lililolipuka kwenye gari.
somalia
Watu kumi walikufa wakati kundi la kiislamu la wapinganaji la Somalia Al Shabaab waliposhambulia jengo la bunge wiki sita zilizopita.
Kundi la Al shabaab lilipoteza udhibithi katika mji mkuu wa Mogadishu tangu mwaka 2011 na tangu wakati huo limekuwa likiendesha mashambulizi ya mabomu na kufanya mauaji.
Mapema wiki hii Mbunge maarufu Ahmed Mohamud Hayd, aliuawa kwa kupigwa risasi katika mji huo, katika shambulio linalodaiwa kufanywa na Al Shabaab

Hii ndio sababu ya Katy Perry kushtakiwa na marapa wa nyimbo za Injili.

katyNyota wa muziki kutoka nchini Marekani Katy Perry ameshtakiwa na marapa nyota wa nyimbo za Injili akiwemo mwanamuziki Flame ambaye amedai kuwa nyimbo ya Dark Horse ya Katy imeiba baadhi ya mistari kutoka kwenye nyimbo yao ya Joyful Noise.
Wanamtuhumu Katy Perry kwa kutumia nyimbo yao iliyotoka mwaka 2008 waliyomshirikisha Lecrae bila ruhusa na kuharibu ujumbe wa kidini uliopo ndani ya nyimbo hiyo na kutumia picha za “kichawi” na nguvu za kidunia.
katyperry
Nyimbo ya Dark Horse iliongoza katika chati za muziki za Billboard kwa wiki kadhaa mwezi January.
Kundi la marapa wa nyimbo za injili Flame aka Marcus Gray, Lecrae Moore, Emanuel Lambert na Chike Ojukwu wanataka kulipwa fidia na mwanamuziki huyo,, studio yake ya Capitol, na waandishi wa nyimbo Dr Luke na Max Martin kwa kuiba hakimiliki za wimbo wao

MTOTO MWENYE MIGUU MITATU KUFANYIWA UPASUAJI

anapaula
Mtoto mdogo ambaye amezaliwa na miguu mitatu amesafirishwa kwenda nchini Marekani kwa ajili ya kufanyiwa upasuaji kuondoa miguu miwili
Ana Paula mwenye miezi 22 alikuwa ni pacha aliyeungana ambapo dada yake hakuweza kupona wakati wa upasuaji wa kuwatenganisha.
ana-paul-1
Ni mguu mmoja tu wa mtoto huyo unaofanya kazi hivyo upasuaji atakaofanyiwa katika moja ya hospitali za watoto ni kuondoa miguu miwili ambayo haifanyi kazi na kumwongezea uwezo wa viungo vyake kufanya kazi.
Ana na mama yake walisafirishwa kutoka Panama kwa msaada waliopatiwa na wasamaria ili zoezi zima liweze kukamilika.
anap2

MJANGA BRAZILI DARAJA LAANGUKA LAUA

daraja2
Tukio hilo limetokea katika mji wa Belo Horizonte wakati magari yakipita chini ya daraja ambapo moja ya malori lililokuwa limebeba gari na ujenzi na gari moja lilinasa kwa mujibu wa maafisa.
daraja3
daraja4

BOMU JINGINE ARUSHA


Majeruhi wa bomu la mkono Arusha

KIONGOZI wa Taasisi ya Answaar Muslim Youth Centre Kanda ya Kaskazini, Sheikh Sudi Ally Sudi, amejeruhiwa kwa bomu la kurushwa kwa mkono akiwa nyumbani kwake Mtaa wa Majengo jijini Arusha.
Aidha, mkazi wa Sinza jijini Dar es Salaam, Muhaji Hussein (38), alipatwa na mkasa huo akiwa nyumbani kwa Sheikh Sudi akitokea safarini Nairobi, Kenya.
Katika mkasa huo, Muhaji alivunjika mguu wa kushoto na kukatika vidole vitatu vya mguu wa kulia kutokana na mlipuko huo.
Ilielezwa kwamba, watu wasiojulikana walivunja kioo cha dirisha usiku huo kisha kurusha bomu hilo hadi sehemu walipokuwa wamekaa watu hao.
Hata hivyo, familia ya Sheikh Sudi imesalimika kutokana na kuwa katika chumba kingine ambacho hakikuathiriwa haraka na mlipuko huo.
Akizungumza katika Hospitali ya Mkoa wa Arusha ya Mount Meru alipolazwa, Sheikh Sudi alisema tukio hilo lilitokea wakati wakiwa wanajiandaa kula daku akiwa na mgeni wake, Muhaji.
Sheikh Sudi akizungumza kwa taabu kitandani alipolazwa katika wodi ya majeruhi alidai kabla ya tukio la bomu tayari alishaanza kupokea vitisho vya kupoteza maisha ikiwamo kutishiwa kwa risasi.
“Nimetishiwa mara kadhaa kabla ya tukio hili nilisharipoti katika vyombo vya dola, ila wameniumiza sana bila sababu,” alisema Sheikh Sudi.
Majeruhi mwingine Muhaji ambaye ana majeraha makubwa maeneo yake ya miguu kuanzia chini ya magoti alisema anamshukuru Mungu kwa kumlinda katika tukio hilo.
“Hapa nilipo nimepata majeraha makubwa katika miguu yote miwili, ambapo mguu wa kushoto umevunjika na mguu wa kulia kidole gumba na vidole viwili vinavyofuata vimekatika,” alisema Muhaji na kuongeza:
“Kabla ya mlipuko mwenyeji wangu alikuwa anasimulia jinsi anavyopokea vitisho wakati huo mtoto wake alikuwa akiandaa chakula.
“Bahati mzuri mtoto alikuwa ameshamaliza na kuondoka tulipokuwa ndipo nikasikia kishindo cha kuvunjwa kioo cha dirisha kilichofuatiwa na mlipuko,” alisema.
DAKTARI WA ZAMU
Kwa upande wake daktari wa zamu katika wodi ya majeruhi, Leo Temba, alisema hali za majeruhi wote wawili inaendelea vizuri na tayari walishawapatia huduma zote muhimu.
Akimzungumzia Muhaji alisema ndiye majeruhi aliyekuwa na hali mbaya zaidi kutokana na kuvuja damu nyingi, hata hivyo baada ya kupatiwa matibabu anaendelea vizuri.
“Wagonjwa wangu mpaka wakati huu wanaendelea vizuri, tumefanya jitihada kuokoa maisha yao. Tumewaongeza damu hasa Muhaji.
“Wote tumesafisha vidonda na kuondoa mabaki yote ya chumachuma na kufunga vidonda ili kuepusha damu kuvuja kwa wingi.”
“Muhaji ndio yuko ‘serious’ amevunjika mguu wa kushoto na una vidonda vikubwa ambavyo tumevifunga na tutavishona. Lakini pia mguu wa kulia umeumia kwani vidole vitatu vimekatika, gumba na vidole viwili vya katikati,” alisema Dk. Temba.
MKUU WA MKOA
Akiwa hospitali kuwatembelea majeruhi Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Magessa Mulongo, aliliambia MTANZANIA Jumamosi kuwa uchunguzi wa awali umebainisha mlipuko huo hauna uhusiano wowote na vikundi vya kigaidi vya Al- Qaeda wala Al- Shabaab.
Magessa alisema kwamba upo mgogoro baina ya waumini wa taasisi za dini ya Kiislamu katika Msikiti wa Qiblatein Kandahari eneo la Soko la Kilombero jijini Arusha.
“Lipo tatizo la ndani kati ya waumini wa Kiislamu kwani Sheikh Sudi ametuambia tayari alishapokea vitisho kutokana na kukataa kutumiwa kwa msikiti huo na makundi ya siasa kali yanayoongozwa na Answar Sunna.
“Tunaendelea kuwasaka vijana hawa tutawakamata wote na kuwafikisha mbele ya vyombo ya sheria,” alisema Mulongo.
Kwa upande wake Kamanda wa Polisi Mkoa wa Arusha, Liberatus Sabas, akizungumzia tukio hilo akiwa Hospitali ya Mount Meru alithibitisha kutokea kwa tukio hilo akisema Jeshi la Polisi litahakikisha linawakamata watuhumiwa wote.
“Pale msikitini kuna msuguano mkali kati ya waumini wenye msimamo mkali na wasio na msimamo mkali. Tupo kazini kuwasaka wote waliohusika na kitendo hiki,” alisema Kamanda Sabas.
Kutokea kwa tukio la Sheikh Sudi kurushiwa bomu akiwa nyumbani kwake linakuwa tukio la tano linalohusiana na matukio ya ulipuaji wa mabomu jijini Arusha.
Tukio la kwanza la mlipuko wa bomu kutokea jijini Arusha lilikuwa ni katika Kanisa la Katoliki Parokia ya Mtakatifu Joseph Mfanyakazi,Olasite, kisha kufuatiwa na mlipuko wa bomu la nyumbani kwa Katibu wa Bakwata Mkoa wa Arusha.
Baada ya hapo mlipuko mwingine wa bomu ulitokea kwatika mkutano wa wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), viwanja vya Soweto kisha kufuatiwa na mlipuko wa bomu katika Bar ya Arusha Night Park (a.k.a Matako Bar).
Mlipuko mwingine sasa unakamilisha idadi ya milipuko mitano ya mabomu kutokea jijini Arusha ni huu wa juzi ambapo Sheikh Sudi na mgeni wake wakiwa nyumba usiku walirushiwa bomu lililowajeruhi miguuni.
Kutokea kwa milipuko yote hiyo kulisababisha kupoteza kwa uhai wa watu ambao jumla ya watu tisa walipoteza maisha yao kutokana na milipuko hiyo huku majeruhu wa milipuko yote wakifikia zaidi ya 120,  ambao kwa nyakati tofauti walikuwa wakipatiwa matibabu na kuruhusiwa kuondoka.

GARI LATEKETEA KWA MOTO DAR

Gari aina ya Toyota Starlet limeungua moto siku ya jana Mji Mwema Kigamboni Dar es Salaam siku ya jana. Chanzo cha moto kilitokana na mafundi kuchomelea na Mtungi wa gesi kulipuka.