| Huyu ni Baraka kijana mrefu kitanzania | 
       Inasemekana ni kijana mrefu kuliko wote Tanzania. Kijana huyu (katikati 
pichani) ambaye anadhaniwa ni mrefu kuliko vijana wote Tanzania anaishi 
maeneo ya Gongolamboto, Banana jijini Dar es salaam. Kijana huyu huwa 
haonekani sana mitaani, lakini aliingia mjini siku hiyo na kuleta kizaa 
zaa kikubwa pale alipoibuka mitaa ya Aggrey, Kariakoo. Alikuwa kivutio 
kwa kila aliyemuona, alifunga mtaa watu wakimshangaa na kumgombania 
kupiga nae picha. Kila aliyetaka kupiga nae picha alitoa Shilingi elfu 
moja Tsh. 1000. 
Picha hiyo amepigwa ndani ya Kinyozi (Salon) aliyoingia kupunguza nywele
 zake na umati wa watu walikuwa nje ya kinyozi huyo kumsubiri atoke. 
Mpaka sasa hajajulikana jina lake kamili na anafanya nini. Inasemekana 
kuna watu wanamfuatilia kumsaidia umaarufu.
|  | 
| Hapa Hasheem Thabit alipokutana na Baraka | 
|   | |
| JULIUS CHARLES | 
UKIMUANGALIA kwa mara ya kwanza mchezaji wa Tanzania anayecheza 
timu ya kikapu ya Oklahoma City Sounders inayoshiriki Ligi ya Kikapu 
Marekani (NBA), Hasheem Thabit unaweza kujiridhisha kwamba ni mrefu 
kuliko Watanzania wote uliowahi kuwaona. Ana futi 7.3.
Lakini mjini Bagamoyo katika Mkoa wa Pwani kwenye 
shule ya Lord Barden yupo mchezaji anayemzidi Hasheem kwa urefu akiwa na
 futi 7.5. Si mwingine namzungumzia Julius Charles (18) ni maarufu zaidi maeneo ya 
Bagamoyo, na umaarufu huo umetokana na kimo chake huku wengi wakimuita 
mpinzani wa Hasheem Thabit  kutokana na urefu alionao ambao umepitiliza 
na ukikutana naye lazima utishike au ubaki ukimshangaa
 
No comments:
Post a Comment