
Rais wa Ukraine aliyeondolewa madarakani Victor Yanukovych amefunguliwa mashtaka
Ukraine imetoa hati ya kukamatwa
 kwa Rais aliyeondolewa madarakani, Victor Yanukovych, Waziri wa mambo 
ya ndani wa mpito ametangaza hatua hiyo.
Arsen Avakov amesema katika ukurasa wa Facebook 
amesema kesi dhidi yake imefunguliwa dhidi ya Yanukovych na maafisa 
wengine kuhusu mauaji ya makubwa ya watu.Wabunge walipiga kura kumuondoa Yanukovych siku ya jumamosi baada ya maandamano ya miezi kadhaa yaliyojitokeza baada ya kupinga kujiunga na Umoja wa Ulaya.
Machafuko yaliyotokana na maandamano hayo yalisababisha watu kadhaa kupoteza maisha juma lililopita.
Avakov amesema Yanukovych alionekana mjini Balaklava siku ya jumapili, lakini mpaka sasa hajulikani mahali alipo.
BBC
 
No comments:
Post a Comment