 
Wizara
 ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa inapenda kukanusha taarifa 
za uvumi zinazosambazwa kwenye mitandao mbalimbali ya kijamii na vyombo 
vya habari kuwa kuna Watanzania wapatao 160 wamenyongwa nchini China kwa
 kosa la kusafirisha madawa ya kulevya.
Wizara inapenda kuujulisha Umma kuwa hakuna Mtanzania yeyote aliyenyongwa kama inavyodaiwa kwenye mitandao na vyombo vya habari.
Aidha, taarifa hiyo ya uvumi imedai kuwa ndugu wa mmoja wa Watanzania hao ambaye kwa jina anajulikana kama Bw. Rajab Mohamed Ismail Mapusa wamekaa matanga kuomboleza kifo chake.
Kwa mujibu wa taarifa rasmi kutoka Serikali ya China, Bw. Mapusa yupo
 hai gerezani akitumikia kifungo cha maisha kwa kosa la kuingiza madawa 
ya kulevya nchini humo, na hivi karibuni alishiriki kuandaa maonyesho ya
 utamaduni wa Kiafrika wakati wa kuadhimisha sherehe za Mwaka Mpya wa 
China.
Wizara
 inapenda kuwakumbusha Wanahabari kuandika taarifa ambazo ni sahihi 
zisizopotosha Umma kwa kuzingatia weledi, maadili na ukweli kutoka 
mamlaka zote husika.
Imetolewa na: Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Dar es Salaam
10 Februari, 2014
 
No comments:
Post a Comment