Watu saba
 wamefariki dunia katika matukio sita tofauti mkoani Iringa likiwemo la 
watoto wawili kufariki wakiwa wanaogelea kwenye dimbwi la maji lililopo 
kijiji cha Mkungugu tarafa ya Isimani.
Akizungumza 
 ofisini kwake kaimu kamanda wa polisi Mkoani Iringa Mratibu mwandamizi 
Peter Kakamba alithibitisha kutokea kwa tukio hilo lililotokea mnamo 
tarehe 23 februari majira ya saa 12:30 jioni.
Kaimu Kakamba aliwataja watoto hao ni Nestory Luhala(8) ambaye ni mwanafunzi wa darasa la pili pamoja na Junior Luhala(5).
Tukio 
lingine mwanafunzi wa miaka 14 ajulikanaye kwa jina la Iginasi 
Ngalembule mkazi wa Isuka  kata ya Mtitu wilayani Kilolo afariki dunia 
baada ya kupigwa na radi.
Kaimu Kakamba alithibitisha kutokea kwa tukio hilo lililotokea mnamo tarehe 22 februari majira ya saa 11 kamili jioni.

 
No comments:
Post a Comment