
Dodoma. 
Wizara ya Fedha imepigilia msumari maombi ya wajumbe wa Bunge Maalumu la
 Katiba ya kutaka waongezewe posho na kusema anayeona ameacha kazi 
inayomlipa zaidi kwenda bungeni afungashe virago na kuondoka.
Msimamo 
huo umekuja siku moja tu baada ya gazeti hili kudokeza kuwa madai ya 
wajumbe wa bunge hilo kutaka waongezewe posho kutoka Sh300,000 za sasa 
kwa siku, yamegonga mwamba baada ya kamati iliyoteuliwa kuchunguza 
uhalali wake kusema kiwango hicho kinatosha.
Mwenyekiti
 wa muda wa bunge hilo, Pandu Kificho alisema jana bila kutaja viwango, 
kuwa ripoti ya kamati hiyo imewasilishwa kwa Rais Jakaya Kikwete kwa 
uamuzi.
 
No comments:
Post a Comment