
Moses mwanamume anayeshiriki mapenzi ya jinsia moja atafuta hifadhi nchini Marekani
                        
Rais wa Uganda Yoweri Museveni 
ametia saini mswada wenye utata unaotoa adhabu kali kwa watakaopatikana 
wakishiriki mapenzi ya jinsia moja.
                     Rais Museveni alitia saini mswada huo nyumbani 
kwake katika hafla iliyoshuhudiwa na maafisa wakuu wa serikali pamoja na
 wandishi wa habari. Adhabu ya maisha jela itatolea kwa watu watakaopatikana na hatia ya kushiriki mapenzi ya jinsia moja zaidi ya mara moja kati ya watu wawili waliokubaliana kufanya hivyo.
Adhabu hiyo pia itatolewa kwa wale wanaopatikana na hatia ya kuwahusisha watoto katika vitendo hivyo, walemavu au kumuambikiza mtu virusi vya Ukimwi.
Mswada huo umepigiwa debe sana nchini Uganda, lakini mashirika ya kimataifa ya kutetea haki za binadamu yameulaani.
 
No comments:
Post a Comment