Thursday 24 April 2014

MWENYEKITI WA CHADEMA AFUNGWA MIAKA 7 KWA KUJERUHI KILABUNI

Mwenyekiti wa CHADEMA Ezekiel King akiteta jambo na jamaa zake mara baada ya kuhukumiwa kwenda jela miaka 7 kwa kosa la kumjeruhi mtu kilabuni
Askari polisi wakimsindikiza Mwenyekiti wa CHADEMA baada ya kuhukumiwa kifungo cha miaka 7 jela

Mmoja wa jamaa waliohudhuria mahakamani akimwaga machozi baada ya Mwenyekiti wa CHADEMA mtaa wa Itiji kuhukumiwa kifungo  cha miaka 7 kwa kujeruhi
 MWENYEKITI wa serikali ya Mtaa wa Itiji Jijini Mbeya mkoani Hapa anayewakilisha (CHADEMA) Ezekiel King(52) na mwenzake Antony Simon(53) wamehukumiwa kwenda jela miaka 7 kutokana na makosa ya shambulio na kumdhuru mwili Nicholaus Mwakasinga(56) mkazi wa Itiji mjini humo.

Akisoma hukumu hiyo Hakimu mkazi wa mahakama ya Mkoa wa Mbeya Maria Batulaine, mbele ya mwendesha mashtaka wa serikali Juliana William alisema kuwa washitakiwa kwa pamoja walimshambulia Mwakasinga kwa kumpiga na kumjeruhi kichwani na mkononi wakati wakiwa katika kilabu cha pombe za kienyeji kilichopo mtaa wa Itiji.

Alisema anawatia hatiani washitakiwa hao kutoka na kuwepo kwa mashaka juu ya ushahidi wa watu watatu  upande utetezi kugongana na hivyo kuridhika na ushahidi wa mashahidi wa upande wa mashtaka na hivyo kuwatia hatiani na kwamba hata hivyo wanayo fursa ya kukata rufaa iwapo hawajaridhika na hukumu iliyotolewa.

Akitoa mifano ya kesi  mbalimbali zinazoshabihiana na kesi hiyo Hakimu Batulaine alisema kuwa makosa hayo ni kinyume cha kifungu sheria  cha kanuni ya adhabu namba 225 sura ya 6 iliyofanyiwa marekebisho mwaka 2002.

Hakimu Batulaine alisema kuwa katika maelezo ya shahidi namba moja Mwakasinga  ambaye ndiye mlalamikaji  ni kwamba alijeruhiwa na kuumizwa na washitakiwa alipoingia katika kilabu cha pombe za kienyeji na  kwamba alifanyiwa hivyo baada ya kuingia ndani ya kilabu hicho na kusukumwana kuanguka nje.

Alisema katika maelezo hayo shahidi namba moja hadi namba tatu wa upande wa mashtaka walitoa ushahidi unaofanana lakini maelezo ya mashahidi wa upande wa utetezi yanajichanganya na hivyo kutoa mashaka juu ya utetezi wao.

Awali ilidaiwa mahakamani hapo kuwa mlalamikaji Mwakasinga alipigwa na kujeruhiwa na washitakiwa na baadaye washitakiwa hao walimchukua na kumpeleka kituo cha Polisi wakidai kuwa mlalamikaji Mwakasinga alikuwa akifanya vurugu kilabuni
.
Hata hivyo mlalamikaji ambaye alilazwa katika hospitali ya rufaa wodi namba nne ambayo hulazwa watu wenye ugonjwa wa akili ili kumpima kama alifanya vurugu kutokana na ugonjwa wa akili alipotoka alifungua mashtaka ya kupigwa na washitakiwa hao ambao walikamatwa na kufunguliwa kesi ya kudhuru mwili.

Katika utetezi wake kabla ya kutolewa hukumu Mshitakiwa King aliomba mahakama impunguzie adhabu kutokana na kuwa na watoto sita na kuwa hakujua kama kitendo cha yeye kama kiongozi wa mtaa kuamka kwenda kwenye tukio kingemtia hatiani

TAZAMA MAFURIKO HUKO KYELA ENEO LA KAJUJUMELE YALIVYO LETA SHIDA, MH. MWAKYEMBE(MB) ATUA HUKO .

Mbunge wa Kyela Dr. Mwakyembe akikagua Barabara iendayo Bandari ya Kiwira
 Baadhi ya watu wakigangaika kupita juu ya maji hayo yaliyotokana na Mafuriko

 Baadhi ya watu mbalimbali wakiwa wanashuhudia Mafuriko hayo muda huu
 Gari Likiwa limekwama katika tope lililotokana na Mafuriko hayo, hili ni eneo la Bujonde 


IDADI YA WALIOKUFA AJALI YA BASI LA LUHUYE YAONGEZEKA



 
Basi la abiria la Luhuye Express lenye namba za usajili T 410 AWQ baada ya kuacha njia na kugonga nyumba katika Kijiji cha Yitwimila 'A', wilayani Busega, Mkoa wa Simiyu .
Wananchi wakishuhudia ajali hiyo
 
Basi la abiria la Luhuye Express baada ya kupinduka.
 
Baadhi ya majeruhi katika ajali hiyo mbaya.
Idadi ya abiria waliokufa kutokana na ajali ya basi la Kampuni ya Luhuye katika Wilaya ya Busega, mkoani  Simiyu juzi imeongezeka kutoka 12 hadi 17.

Baadhi ya marehemu, akiwamo Mchungaji wa Kanisa la Waadiventista Wasabato (SDA) Wilaya ya Kahama, mkoanim Shinyanga, wametambuliwa.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Simiyu, Charles Mkumbo, alisema wawili kati yao, walifariki  juzi jioni wakati wakiendelea kupatiwa matibabu katika Hospitali ya Rufaa Bugando.

Hata hivyo, Kamanda Mkumbo alisema Jeshi la Polisi linamshikilia mmiliki wa basi hilo, Masalu Jackson (37)mkazi wa eneo la Majengo mapya, Wilaya ya Bunda, mkoani Mara,  kwa ajili ya upelelezi wa kipolisi.

Kwa mujibu wa Kamanda Mkumbo, baadhi ya maiti na majeruhi bado hawajatambuliwa hadi kufikia jana jioni.

Aliwataja maiti waliotambuliwa kuwa ni Mchungaji huyo wa SDA, Thomas Mwita (40), naAfisa Elimu wa Shule Msingi wa Halmashauri ya Wilaya ya Shinyanga, Mkoa wa Shinyanga, Wangwe Maurice ( 30), ambao walikuwa wakitibiwa katika Hospitali ya Wilaya ya Magu.

Aliwataja wengine,  ambao pia walikuwa  wakitibiwa katika Hospitali ya Wilaya ya Magu  kuwa ni Mahemba Chacha (42), mkazi  wa Wilaya ya Serengeti, mkoani Mara, Rahma  Kibera (32) mkazi wa Bugalika, jijini Mwanza, Alex  Masatu (42).

Ingawa hakutaja majina, Kamanda Mkumbo alisema majeruhi tisa waliokuwa   wamelazwa Hospitali ya Wilaya ya Magu wametambuliwa na kwamba, wawili kati yao,  hali zao ni mbaya.

“Majeruhi 33 waliofikishwa Hospitali ya Rufaa Bugando kwa ajili ya matibabu, bado  wamelazwa. Wengine wawili, Esther Moris (18) mkazi wa Sirari, wilayani Tarime, mkoani Mara na Rose Wilson (21) mkazi wa Igoma, jijini Mwanza walifariki jana jioni  baada ya kuwa nimetoa taarifa za awali kwa vyombo vya habari,” alisema.

Aliwataja wengine waliokufa jana wakati wakitibiwa katika Hospitali ya Rufaa Bugando  kuwa ni Sheta Msongoma (58), mkazi wa Nassa, Jimbo la Busega, mkoani Simiyu na mtoto mwenye umri wa mwaka mmoja, Baraka Alex.

“Tusaidiane kutoa wito kwa watu wa mbali wajitokeze kwa wingi katika hospitali hizi mbili; Magu na Bugando ili wawatambue ndugu zao,”  alisema Kamanda Mkumbo.

KIKWETE ATUMA RAMBIRAMBI
Rais Jakaya Kikwete, amemtumia salamu za rambirambi Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Paschal Mabiti, kufuatia vifo vya watu 17 waliopoteza maisha yao katika ajali ya basi hilo.

Katika salamu hizo, Rais Kikwete amesema kuwa ni jambo la kusikitisha kuwa ajali za barabarani zinaendelea kuchukua maisha ya watu wasiokuwa na hatia.

“Nimepokea kwa huzuni nyingi taarifa ya ajali hiyo ambayo nimejulishwa kuwa imetokea katika kijiji cha Itwimila katika Wilaya ya Busega katika Mkoa wako wa Simiyu wakati basi lililokuwa linasafiri kutoka Tarime, Mkoa wa Mara kwenda Mwanza kupitia Simiyu lilipoacha njia na kugonga nyumba kabla ya kupinduka.”

“Nakutumia salamu zangu za rambirambi na najiunga nanyi katika kuomboleza msiba huu mkubwa katika nchi yetu. Aidha, kupitia kwako, natuma salamu za dhati ya moyo wangu kwa familia zote ambazo zimepoteza wapendwa wao katika ajali hiyo.

Naungana nao katika kuomboleza wapendwa wao. Napenda wajue kuwa msiba wao ni msiba wangu. Pia, naungana nao katika kumwomba Mwenyezi Mungu, Mwingi wa Rehema aziweke peponi roho za marehemu, alisema Rais Kikwete.”

Pia Rais Kikwete ametoa pole kwa wote ambao wameumia katika ajali hiyo, akiwaombea wapone haraka na kurejea kwenye shughuli zao za kujiletea maendeleo

RAIS KIKWETE AZINDUA UJENZI WA HOSPITALI KUBWA NA YA KISASA YA CHUO KIKUU CHA AFYA NA SAYANSI SHIRIKISHI MUHIMBILI KIJIJINI MLOGANZILA

Rais Dkt Jakaya Mrisho Kikwete akipeana mikono na Balozi wa Korea nchini Mhe Chung IL wakiwa mbele ya mchoro wa mfano wa Hospitali ya Chuo Kikuuu cha Afya na Sayansi Shirikishi cha Muhimbili kijijini Mloganzila maeneo ya Kwembe, Kilometa 25 kutoka jijini Dar es salaam, baada ya kuweka jiwe la msingi la ujenzi wa hospitali hiyo itakayokuwa kubwa kuliko zote nchini leo
Rais Dkt Jakaya Mrisho Kikwete akifurahi na msanii Mrisho Mpoto baada ya kuweka jiwe la msingi la ujenzi wa  Hospitali kubwa na ya kisasa ya Chuo Kikuuu cha Afya na Sayansi Shirikishi cha Muhimbili kijijini Mloganzila maeneo ya Kwembe, Kilometa 25 kutoka jijini Dar es salaam, baada ya kuweka jiwe la msingi la ujenzi wa hospitali hiyo itakayokuwa kubwa kuliko zote nchini
Rais Dkt Jakaya Mrisho Kikwete na Balozi wa Korea nchini Mhe. Chung IL  wakikata utepe kuashiria uwekaji wa  jiwe la msingi la ujenzi wa  Hospitali kubwa na ya kisasa ya Chuo Kikuuu cha Afya na Sayansi Shirikishi cha Muhimbili kijijini Mloganzila maeneo ya Kwembe, Kilometa 24 kutoka jijini Dar es salaam, baada ya kuweka jiwe la msingi la ujenzi wa hospitali hiyo itakayokuwa kubwa kuliko zote nchini leo April 24,  2014
Rais Dkt Jakaya Mrisho Kikwete na Balozi wa Korea nchini Mhe. Chungh IL wakiweka udongo kwa pamoja wakati wa kuweka  jiwe la msingi la ujenzi wa  Hospitali kubwa na ya kisasa ya Chuo Kikuuu cha Afya na Sayansi Shirikishi cha Muhimbili kijijini Mloganzila Kilometa 25 kutoka jijini Dar es salaam, 
Rais Dkt Jakaya Mrisho Kikwete na Balozi wa Korea nchini Mhe. Chung IL na viongozi wengine  wakikata utepe kuashiria uwekaji wa  jiwe la msingi la ujenzi wa  Hospitali kubwa na ya kisasa ya Chuo Kikuuu cha Afya na Sayansi Shirikishi cha Muhimbili kijijini Mloganzila maeneo ya Kwembe  Kilometa 25 kutoka jijini Dar es salaam,
Rais Dkt Jakaya Mrisho Kikwete akimkabidhi mkasi Mbunge wa Ubungo (CHADEMA) Mhe John Mnyika ili na yeye akate utepe na viongozi wengine kuashiria uwekaji wa  jiwe la msingi la ujenzi wa  Hospitali kubwa na ya kisasa ya Chuo Kikuuu cha Afya na Sayansi Shirikishi cha Muhimbili kijijini Mloganzila mkoa wa Pwani leo April 24,  2014.
Rais Dkt Jakaya Mrisho Kikwete akiongea katika sherehe za kuweka jiwe la msingi la ujenzi wa  Hospitali kubwa na ya kisasa ya Chuo Kikuuu cha Afya na Sayansi Shirikishi cha Muhimbili kijijini Mloganzila mkoa wa Pwani leo April 2014.

PICHA NA IKULU

Rekodi iliyowekwa na kiatu cha Cristiano Ronaldo alichovaa jana dhidi ya Bayern Munich

Real Madrid v FC Bayern Muenchen - UEFA Champions League Semi FinalUsiku wa jana kwenye mchezo wa ligi ya mabingwa ulaya kati ya Real Madrid vs Bayern Munich mshambuliaji Cristiano Ronaldo alirudi uwanjani baada ya kukosekana kwa takribani wiki mbili uwanjani.
Pamoja na kurudi kwake na kuisaidia timu yake kushinda jana, lakini Ronaldo jana alitengeneza headlines kwa kiatu kipya cha kucheza alichovaa.
10299923_699658110097071_8417158352982918543_n
Ni kiatu kipya alichotengenezewa na kampuni ya Nike kilichotengenzwa kwa kuwekwa rangi ilitokana na dhahabu na ngozi nyeupe kilianza kuuzwa jana kwenye mtandao wa Nike.com lakini ndani ya sekunde kadhaa tu kiliuzwa stock yote – kiatu hiki ni limited edition na vilitengeneza viatu pea 100 tu.
Nike Cristiano Ronaldo 2014 Special Edition Boot Gold Clasico(1)
Kiatu kilichopewa jina la mercurial vapor ix cr7 white / black / gold kilikuwa kikiuzwa kwa kiasi cha 310 USD (235 Euro).

Taarifa kuhusu kocha mpya wa Taifa Stars na lini anakuja Bongo

KOCHAKocha Mkuu mpya wa Taifa Stars, Martinus Ignatius Maria maarufu kama Mart Nooij anatarajiwa kuwasili nchini Jumamosi alfajiri (Aprili 26 mwaka huu) tayari kwa ajili ya kuanza kazi ya kuinoa timu hiyo.

Nooij (59) atawasili saa 7.20 usiku kwa ndege ya Ethiopia Airlines ambapo anatarajia kukutana na waandishi wa habari Jumamosi mchana, saa chache kabla ya kuanza mechi ya kirafiki kati ya Taifa Stars na Burundi itakayochezwa kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.
Mart Nooij ni raia wa Uholanzi, na ameshawahi kufanya kazi katika nchi ya Mozambique kama kocha mkuu wa timu ya taifa, Burkina Faso U20, na pia ameifundisha timu ya Santos ya Afrika ya Kusini

Monday 21 April 2014

Maneno ya Meneja wa Uwanja wa Taifa,baada ya kukutwa mayai 3 uwanjani.

yaiiMechi ya watani wa jadi Simba na Yanga ambayo ilichezwa April 19 imeingia kwenye headline baada ya kuhusishwa na imani za kishirikina na hii ni baada ya kufukuliwa kwa mayai 3 uwanja wa taifa jijini Dar es salaam.
Urio ambaye ni Meneja wa Uwanja wa taifa amepatikana kulizungumzia hili ameanza kwa kusema>>’Unajua mambo yanayohusiana na mambo ya kishirikina kwanza Serikali haiyaamini,wanaozungumza mambo ya kishirikina siwezi kuwakataza kuzungumza kwa sababu kila mtu ana imani yake lakini sisi vitu hivyo hatujihusishi,hatuvutaki na hatutojihusisha nayo kabisa kwa sababu hayako kwenye imani zetu na sio sehemu ya kazi’
‘Ni uongo kabisa vitu vifukuliwe uwanjani kama waliona na kama mtu aliingia nalo yai huwezi kumwambia mtu hakukaguliwa kwa sababu yai hata ukipita kwenye vile ving’amuzi vya polisi haviwezi kung’amua kwa sababu yai sio chuma hivyo haviwezi kupiga kelele lakini hiyo mimi siwezi kuelezea kwa sababu sijasikia mambo ya mayai wala kusikia sijaona vitu vya uchawi lakini nimesikia watu wanazungumza’
‘Hii ipo kwenye michezo yote unayaikia ooh wameroga hawa wamefanya hivi na huwezi kuwazuia watu kusema kwenye uwanja mpya wa Taifa haijawahi kutokea’.

Picha 3 jinsi bondia mtanzania Francis Miyeyusho alivyochapwa round ya kwanza kwa KO


IMG_1776
Pambani hili limefanyika kwenye ukumbi wa PTA ambapo bondia Francis Miyeyusho amepigwa na bondia kutoa Thailand Sukkasem Kietyongyuth kwenye raundi ya kwanza kwa knock out.
Bondia huyo wa Thailand amempiga Miyeyusho dakika ya kwanza na sekunde 54 na kwenye hizo dakika alianguka mara kadhaa hadi refa anampa ushindi mthailand huyo.
IMG_1749

IMG_1776

IMG_1777

Picha na Seleh Jembe

Kurasa za mbele na nyuma kutoka kwenye magazeti ya leo April 21

IMG_20140421_100707
IMG_20140421_105328
IMG_20140421_105312
IMG_20140421_105303
IMG_20140421_105253
IMG_20140421_105143
IMG_20140421_105150
IMG_20140421_105223
IMG_20140421_105233
IMG_20140421_105245
IMG_20140421_105125
IMG_20140421_105113
IMG_20140421_105057
IMG_20140421_105048
IMG_20140421_105035
IMG_20140421_104919
IMG_20140421_105143
IMG_20140421_100650
IMG_20140421_104933
IMG_20140421_104951
IMG_20140421_105057
IMG_20140421_100730
IMG_20140421_105002
IMG_20140421_105113
IMG_20140421_105125
IMG_20140421_100745
IMG_20140421_105027
IMG_20140421_105303