Kuna mambo mengi yamezungumzwa tangu jana na hadi leo kuhusu matokeo ya uchaguzi wa marudio katika kata 27 na ushindi wa CHADEMA katika kata 3 za Kiborloni, Sombetini na Njombe mjini.
Tutaendelea 
kusoma, kusikiliza na kupokea kila aina ya criticism, zinazotolewa kwa 
njia mbalimbali, ingawa hatimaye tutafanyia kazi constructive criticism 
zinazojengwa katika dhamira ya kweli na nia njema kwa ajili ya 
mustakabali wa Watanzania na chama chao, CHADEMA.
Moja ya 
masuala yanayozungumzwa na wapinzani wa CHADEMA, ambayo hata leo katika 
press conference iliyoitishwa Lumumba, litazungumza sana, ni kujaribu 
'kuoanisha' M4C-OPD (matumizi ya chopa 3) na ushindi wa kata 3.
Kuoanisha 
mambo hayo kwa mgongo wa kufanya uchambuzi au tathmini ya mambo hayo 
mawili, ni ama kuamua kuwa myopic kwenye hoja muhimu au kuamua kupotosha
 kwa makusudi ya propaganda nyepesi au kutokujua tu.
Wakati 
Mwenyekiti Mbowe anazindua M4C- Operesehni Pamoja Daima, mbele ya 
waandishi wa habari alisema malengo ya shughuli hiyo maalum kuwa itaweka
 msisitizo au mkazo kwenye masuala makuu yafuatayo;
- Mchakato wa katiba mpya Daftari la wapiga kura Wazawa na rasilimali za nchi yao Ugumu wa maisha unaosababishwa na uongozi mbovu na sera zilizoshindwa za CCM
Kwa wale 
waliofuatilia OPD, kila mtu anajua namna ambavyo imeibua mjadala mkali 
katika masuala hayo, kuanzia na katiba mpya, wazawa na matumizi 
(unufaikaji) ya rasilimali, ugumu...
Tume ya 
Taifa ya Uchaguzi ikalazimika kutangaza kwamba tayari serikali imetoa 
fedha za kuboresha daftari la wapiga kura. Haitoshi tu kusema hivyo. 
Viongozi wakuu, Mwenyekiti Mbowe na Katibu Mkuu Dkt. Slaa wakatoa kauli 
ya chama wakiitaka NEC itoe taarifa kamili juu ya mambo kadhaa, ikiwa ni
 pamoja na;
- Ratiba kamili ya shughuli hiyo Lini NEC itaanza kukagua vituo Tarehe rasmi ya kuanza kuboreshwa daftari Serikali imetoa bajeti ya kiasi gani (inatosha kwa shughuli nyeti kama hiyo?
Kwa sababu 
M4C-OPD ilikuwa ni ya nchi nzima, yako maeneo ya uchaguzi ambako chopa 
zilifika. Lakini kuoanisha matumizi ya chopper 3 na matokeo ya ushindi 
wa kata 3, ni kulazimisha hoja isiyokuwepo kwa premises za 
kuokoteza Wapinzani wa CHADEMA wakisukumwa na euphoria ya ushindi 
usiokuwa na uhalali (tutafafanua), wamejikita kwenye 'negative (ya 
picha)' inayozungumzia chopper 3 kwa kata 3, wanashindwa kuiona 'picha 
kubwa' (negative Vs bigger picture), inayozungumzia masuala kadhaa, 
mfano;
Katika uchaguzi wa 2010 matokeo yalikuwaje?
Je kuna mabadiliko ya goal post, figures na namba?
Je mabadiliko hayo yako in favour of status quo au yanasapoti vuguvugu la mabadiliko?
CHADEMA 
itajikita katika hayo kwa sababu ni muhimu sana katika suala kulinda 
demokrasia ya watu na kusheherekea ushindi, hasa ushindi ulio halali.
Mfano; 
katika Kata ya Njombe mjini, mwaka 2010 CHADEMA haikusimamisha mgombea 
kabisa wa udiwani wala ubunge. Mgombea Urais wa CHADEMA alimzidi kwa 
mbali mno mgombea urais wa CCM. Mbali mno.
Matokeo ya jana katika kata hiyo hiyo kwa uchaguzi wa udiwani, yanaonesha kwamba;
CHADEMA imepata kura 2,202 CCM imepata kura 1,094
Jumla ya kura zilikuwa 3334
Jumla ya vituo vilikuwa 41, CCM imeshinda kituo kimoja tu kwa tofauti ya kura 9
Iko mifano mingi ya 
namna hii katika uchaguzi wa jana. Kuna maeneo ambayo CHADEMA haikuwahi 
kuweka mgombea, imetoa ushindani mkali na kuna maeneo ambayo uchaguzi 
uliopita kulikuwa na tofauti kubwa mno ya kura, lakini safari hii gap 
limepunguzwa kwa namba kubwa sana. 
Mfano Kata ya Mpwayungu, Mtera, Dodoma Mwaka 2010
CHADEMA 602
CCM       1812 
Mwaka 2014 (jana)
CHADEMA 555
CCM         872
Katika Kata ya Ubagwe, mwaka 2010, CCM ilipita bila kupingwa. Uchaguzi wa jana umekuwa;
CCM 329
CHADEMA 215
TADEA 71
Zilizoharibika 3
Where are the voters? Where is legitimacy? 
Moja ya masuala ya msingi sana ambayo tulitarajia yawaumize kichwa sana watu, hususan walioko madarakani ni swali hili; Je wapiga kura wako wapi?
Suala hili limepewa uzito na CHADEMA pamoja na wapenda demokrasia na 
maendeleo wengine wengi tu nchini tangu baada tu ya matokeo ya uchaguzi 
mkuu wa mwaka 2010. Nani anajali?
Walioko madarakani wangelikuwa wanathamini mchakato wa demokrasia ya 
uwakilishi, ambayo maana yake ni kuwaheshimu watu/wapiga kura, kamwe 
wasingekuwa wanakimbilia kushangilia matokeo, tena yasiyowapatia 
uhalali.
Mathalani
Kata ya Ubagwe, Ushetu, Shinyanga
Wapiga kura walioandikishwa wako 4270
Waliopiga kura jana ni 618
CCM wameshinda kwa kura 329 dhidi ya CHADEMA kura 215, TADEA- 7, zilizoharibika 3. 
Kata ya Nyasura Bunda, 
Waliojiandikisha ni 5333
Waliopiga kura      1579
Wapiga kura wako wapi? Uko wapi uhalali wa ushindi wa kata nyingi?Aidha,
 wapinzani wa CHADEMA hawataki kabisa kabisa kuzungumzia irregularities.
 Very serious irregularities done purposefully. Hawataki kabisa kugusia 
namna ambavyo watu wamepigwa wazi wazi na kuchukuliwa kwenye vituo vya 
kura, wakiwemo mawakala wa CHADEMA kisha eti wakapelekwa vituo vya 
polisi.
Wapenda demokrasia hao ya ushindi, hawataki kabisa kuzungumzia mapanga na mashoka yaliyotembezwa jana na Green Guards! 
Huwezi kuzungumzia kushindwa au kushinda kwenye matokeo ya jana au 
mengine yoyote yale, bila kujadili masuala hayo kwa upana sana, unless 
kama tumekubaliana kuwa iwe ni sehemu ya demokrasia yetu, watu kukatwa 
mapanga, mashoka, damu kumwagika, watu kukamatwa vituoni bila makosa, 
kisha CCM wakaachwa wanafanya wanavyotaka, wakuu wa wilaya kuingia 
vituoni na kutoa maagizo.
Labda kwao ni sehemu ya mchakato wa kuchagua wawakilishi! Vinginevyo basi tuanze kuwaandaa Watanzania kwa uchafu wa namna hii.
Kwa kusema haya kamwe haimaanishi kuwa CHADEMA haihitaji kufanya 
tathmini ya kitaalamu, kitaaluma na kina sana. Itafanyika na itakuwa 
muhimu kwa ajili ya kuendelea kujiimarisha na kujipanga katika mapambano
 haya. 
Lakini kwa vyovyote ni muhimu sana sana, kuweka mikakati ya kukabiliana na Intarahamwe inayotaka kupandikizwa Tanzania na Watawala dhidi ya Watanzania.
Suala hili la Green Guards kufanya maovu dhidi ya wapinzani wa CCM 
kwenye uchaguzi, tena mahali pengine uovu wa kutisha unaohusisha silaha,
 kwa namna ile ile ya Intarahamwe, mbele ya askari polisi, wala 
wasiguswe, wapo wengine bado wanaliona kuwa ni jambo dogo au mzaha 
fulani hivi.
Siku madhara yake yatakapokuwa yameshafika mfupani, tutajua Intarahamwe ilikuwa ni kitu gani, kilianzaje, kilipataje nguvu na matokeo yake yalikuwa ni nini. 
Where are the voters, where is legitimacy?
Tumaini Makene
Afisa Habari-Chadema

 
No comments:
Post a Comment