Picha juu ni baadhi ya abiria wakiwa kwenye hali  baada ya lori scania namba T653 BFD  (scania 380) kugongana uso kwa uso na baso dogo la abiria Toyota Hiace T613 CPG iliyokuwa inatoka mbagala kwenda mkuranga jana
---
WATU wanne wapo katika hali mbaya na wengine saba wamejeruhiwa baada ya lori scania namba T653 BFD  (scania 380) kugongana uso kwa uso na baso dogo la abiria Toyota Hiace T613 CPG iliyokuwa inatoka mbagala kwenda mkuranga.
Kwa
 mujibu wa shuhuda ya ajali hiyo iliyotokea Mwandege, Dominic Kubhota, 
ameiambia blogu hii usiku huu kwamba chanzo cha ajali hiyo ni ovateki 
isiyotumia akili ya lori hilo . Majeruhi
 hao wamefikishwa katika hospitali ya Mkuranga, lakini muda mfupi 
baadaye walianza kukimbizwa kuleta dare s salaam kw amatibabu zaidi.
Abiria wawili waloikuwa mbele  ya daladala walikatika miguu.
Majeruhi wengine walioweza kuzungumza ni: Mustafa mfungapoa wa mkuranga Abdul Ally wa mwandege Ramadhani rajab Theofrida Mwinuka ( alikuwa mbele amevunjika miguu)Jamal  mbaraka ( aliyekwanguka ngozi ya kichwa)Abraham Mohamed
Swalehe salum
 
No comments:
Post a Comment