Tuesday, 4 February 2014

Hiki ndio alicho post Anderson wa Man U

125448_luis-nani--anderson--wayne-rooney-dan-javier-hernandez_663_382
Jana vyombo vya habari kadhaa barani ulaya viliripoti taarifa kwamba mwanasoka wa kibrazil wa Manchester United Anderson aliyeopo katika klabu ya Fiorentina kwa mkopo, amezungumza na kusema kwamba yeye ameondoka kwa mkopo lakini anataka kuihama kabisa Manchester, huku akitabiri kwamba wachezaji wengi wa timu hiyo wataondoka akiwemo Nani ambaye amechoshwa na timu hiyo.
Lakini kupitia ukurasa wa mtandao wa kijamii wa instagram, Anderson amekana kusema maneno hayo akionekana kushtushwa na taarifa hizo, huku akisema hajawahi kufanya mahojiano na kutamka maneno hayo yaliripotiwa.
f60e96668d2c11e3ae0e12ea8b4c068d_8“Nimeshutushwa na kushangazwa na taarifa hizo, sijawahi kufanya mahojiano na kutamka maneno mabaya kuhusu klabu ninayoipenda, klabu ambayo imenilea na kunifundisha vitu vingi,” ilisema taarifa hiyo ya Anderson.

No comments: