Marekani haikufurahishwa na hatua ya Uganda kuidhinisha sheria dhidi ya wapenzi wa jinsia moja.
Waziri
wa mashauri ya Kigeni wa Marekani, John Kerry amesema tangu Uganda
iidhinishe mswada huo miaka minne iliyopita, Marekani ilieleza wazi
kwamba sheria hiyo inakiuka jukumu la kuhakikisha kuwepo haki za
binaadamu ambalo tume ya haki za binaadamu Uganda inatambua linaambatana
na sheria ya Uganda.
Kerry
amesema,' Baada ya kuidhinishwa sheria hii, tunaanza ukaguzi wa ndani
wa uhusiano wetu na serikali ya Uganda, kuhakikisha kwamba pande zote za
uhusiano wetu, ukiwemo miradi ya msaada, zinapinga sera na sheria
zinazowaonea watu na tuwe na uhusiano unaodhihirisha maadili yetu'.
Tamko
hilo limetolewa siku moja baada ya rais Yoweri Museveni kukaidi
shinikizo la kimataifa na kutia saini sheria hiyo iliyo zusha mzozo,
inayoharamisha mapenzi ya jinsia moja Uganda, hatua iliyozusha hisia
kali.
Baadhi ya mataifa ya magharibi tayari yanatishia kukatiza msaada wa moja kwa moja kwa serikali ya Uganda.
Marekani
inasema kuidhinishwa kwa sheria hiyo kunatishia hatari ya kurudi nyuma
katika uwajibikaji wa Uganda kulinda haki za raia wake na kutishia jamii
ya wapenzi wa jinsia moja Uganda.Chanzo BBC Swahili