Rasimu hiyo ya kanuni inasisitiza kuwa mjumbe
anayeshindwa kufuata taratibu anawezwa kusimamishwa, na hatapokea posho
hiyo kwa kipindi chote atakachokuwa benchi.
Hata hivyo, wabunge mbalimbali walisikika leo
asubuhi wakisema kuwa kiwango hicho cha Sh 220,000 ni kidogo sana, hali
inayofanya washindwe kumudu gharama za maisha mjini Dodoma.
Richard Ndassa (CCM-Sumve) aliiambia Mwananchi
kiwango walichowekewa ni sawa na “posho aliyokuwa akilipwa dereva wa
Tume ya Mabadiliko ya Katiba.” “Hii siyo sawa kabisa,” alisisitiza.
Mbunge wa Kishapu, Suleiman Nchambi alikuwa na
haya ya kusema: “Sisi tumeshazoea maisha ya Dodoma na tunaishi hivyo
hivyo tu licha ya kuwa fedha ni ndogo.”
“Ila hawa wenzetu ambao ni wageni hali zao ni mbaya.”
Katika jitihada za kuzima fukuto hilo la posho,
Mwenyekiti wa muda wa Bunge la Katiba, Pandu Ameir Kificho aliahidi
kulirudisha suala hilo serikalini ili litazamwe upya. NA MWANAINCHI
No comments:
Post a Comment