Friday 14 February 2014

CHADEMA KANDA YA ZIWA YAWAFUKUZA VIONGOZI WAKE WATANO KWA KOSA LA KUMPA USHIRIKIANO ZITTO KABWE

Viongozi waliovuliwa nyadhfa zao ni Mwenyekiti wa jimbo la Kahama Israel Barikiel, Katibu wa Jimbo Vicent Kilukilwa, Katibu Mwenezi wa jimbo Bobson Wambura, Mwenyekiti Bawacha Kasigwa Adram na Mwenyekiti Bavicha Benedict Shija.

Katika Barua yake aliyoiandika kwa viongozi hao, Nzemo amesema viongozi hao wanakabiliwa na tuhuma za kikiuka tamko la kamati kuu ya chama lililowazuaia wanachama wote kushirikiana na aliyekuwa naibu katika mkuu wa chama hicho Zitto Kabwe.



Tuhuma zingine ni kushiriki kampeni za uchaguzi mdogo katika kata ya Ubagwe kupitia chama cha TADEA, huku viongozi hao wakipita na kujinadi kuwa wako tayari kumfuata Zitto popote atakapokuwa.

Aidha Nzemo amesema viongozi hao wamekuwa wakitumia nembo ya CHADEMA kunadi chama kingine cha Alliance for change and Transparency (ACT), kinyume cha maadili ya CHADEMA katika katiba yake ya mwaka 2006.

Nzemo amesema kutokana na tuhuma hizo na zile zilizotolewa na baraza la mashauriano wilaya ya Kahama, viongozi hao wanatakiwa kukabidha ofisi na vifaa vya chama kwa baraza la wazee jimbo la Kahama mara wapatapo barua hizo.


No comments: