Monday 17 February 2014

TAZAMA PICHA ZA MSANII LULU ALIPOKUWA MAHAKAMANI LEO KUSIKILIZA KESI YAKE

Kesi ya kuua bila kukusudia inayomkabili msanii wa kike wa filamu Tanzania Elizabeth Michael maarufu kwa jina la
Lulu akituhumiwa kumua msanii mwenzake wa filamu Steven Kanumba imetajwa leo mahakama kuu kanda ya Dar es Salaam.Mnamo tarehe 7/4/2012 huko sinza vatican Dar es Salaam mtuhumiwa bila makusudi alimua Steven Kanumba.Mshitakiwa na marehemu walikua na uhusiano wa penzi.Siku ya tukio mshtakiwa alienda kumtembelea marehemu nyumbani kwake sinza akawakuta marehemu na mdogo wake Setty Bosco wakijiandaa kutoka saa 12.00pm ya usiku.Ndipo mshtakiwa alifika nakuingia ndani kwenye chumba cha marehemu.Mdogo wa marehemu akasikia malumbano kati ya Lulu na Kanumba kwa nini anapokea simu za watu wengine.Baada ya hapo lulu akataka kutoka nje marehemu akamvuta arudi ndani .Baada ya hapo lulu akatoka nje akiwa analia na kumuambia Setty Kanumba ameanguka chini.Ndipo Setty Bosco akawasiliana na dokta wake kanumba akafika nyumbani na kumfanyia vipimo ikagundulika amefariki dunia lakini dokta hakumuambia mdogo ake kanumba mpaka alipopelekwa muhimbili ikabainika amefariki dunia kutokana na uvimbe ndani ya ubongo.Mshitakiwa alikamatwa Bamaga na kupelekwa kituo cha Polisi cha osterbay.Baada ya kusomewa mashitaka hayo mshitakiwa alikana .Upande wa jamhuri chini ya wakili mwandamizi Monica Mbogo umewasilisha ripoti ya kitabibu na ramani ya tukio pia kutakua na mashahidi watano Setty Bosco,Dr Palpas Kageiya,Esther Zefania na E.6056 Lenatus.Upande wa mshtakiwa wakili Peter Kibatala alisema mashahidi wako watano hakuwataja majina.

Hata hivyo jaji Rose Temba aliyekua anaisikiliza kesi hiyo amehairisha kesi mpaka itakapopangiwa tarehe ya kuanza kusikilizwa rasmi pande zote mbili jamhuri na mshitakiwa watajurishwa.

No comments: