Sunday 9 February 2014

Waziri wa uhamiaji wa Uingereza ajiuzulu



*Waziri wa Uhamiaji wa Uingereza, Mark Harper (pichani), amejiuzulu baada ya kujulikana kuwa amemuajiri mtu asiyekuwa na kibali cha kubaki nchini.* *Alieleza kuwa alidanganywa na mwanamke mmoja aliyemuonesha nyaraka za bandia, alipomuajiri kusafisha nyumba yake.* *Bwana Harper alisema kwa sababu alichangia kupitisha bungeni sheria ngumu kuhusu uhamiaji, alihisi inambidi kuwajibika zaidi kushinda wengine.* *Chama cha Conservative kimeahidi kupunguza idadi ya watu wanaohamia Uingereza kutoka malaki na kuwa elfu kadha tu.* *Chanzo: BBC Swahili*

No comments: