Friday 14 February 2014

ADAKWA NA MENO 21 YA TEMBO YENYE THAMANI YA MIL 43 SINGIDA

JESHI la polisi mkoani Singida limekamata vipande 21 vya meno ya Tembo vyenye thamani ya zaidi ya shilingi milioni 43.Nyara hizo za serikali zimekamatwa katika kijiji cha Mwamagembe wilayani Manyoni  zikisafirishwa kwenda Itigi, mkoani Singida.     

Mtu mmoja  George James amekamatwa kwa tuhuma za kukutwa na meno  hayo ya tembo yakiwa yamehifadhiwa katika mabegi mawili ya kusafiria. Mtuhumiwa huyo alikamatwa katika kizuizi cha idara ya maliasili kilichoko katika kijiji Ukimbu, kata  ya Mgandu, wilayani Manyoni akiwa katika gari aina ya Toyota Hiace lenye namba za usajili T797CQL. 

Kamanda wa polisi mkoa wa Singida RPC Geofrey Kamwela (katika video) amesema vipande hivyo 21 vina thmani ya zaidi ya shilingi milioni 43 na vyote vimehifadhiwa katika kituo cha polisi wilayani Itigi.









No comments: