Monday 24 February 2014

WATU SABA WAFARIKI DUNIA MKOANI IRINGA

 

Watu saba wamefariki dunia katika matukio sita tofauti mkoani Iringa likiwemo la watoto wawili kufariki wakiwa wanaogelea kwenye dimbwi la maji lililopo kijiji cha Mkungugu tarafa ya Isimani.
Akizungumza  ofisini kwake kaimu kamanda wa polisi Mkoani Iringa Mratibu mwandamizi Peter Kakamba alithibitisha kutokea kwa tukio hilo lililotokea mnamo tarehe 23 februari majira ya saa 12:30 jioni.
Kaimu Kakamba aliwataja watoto hao ni Nestory Luhala(8) ambaye ni mwanafunzi wa darasa la pili pamoja na Junior Luhala(5).
Tukio lingine mwanafunzi wa miaka 14 ajulikanaye kwa jina la Iginasi Ngalembule mkazi wa Isuka  kata ya Mtitu wilayani Kilolo afariki dunia baada ya kupigwa na radi.
Kaimu Kakamba alithibitisha kutokea kwa tukio hilo lililotokea mnamo tarehe 22 februari majira ya saa 11 kamili jioni.

No comments: