Monday 24 February 2014

MWANAMKE AKAMATWA AKITUPA MTOTO MCHANGA CHOONI HUKO MBEYA



Rukia Fungameza(20) mkazi wa mtaa wa Ilembo Kata ya Iwambi Anaetuhumiwa kutupa mtoto chooni
 
 Hii ndilo shimo la choo alimotumbukizwa mtoto huyo.

 Wakina mama wakilia kwa uchungu
 
Mwenyekiti wa mtaa huo Juma Mbuza mwenye Flana ya bluu akiwa na barozi kushoto na mashuhuda wengine wakimsikiliza mwenyekiti huyo.
Mwanamke mmoja aliyefahamika kwa jina la Rukia Fungameza[20]mkazi wa mtaa wa Ilembo Kata ya Iwambi anashikiliwa na Jeshi la Polisi Mkoani Mbeya kwa tuhuma za kutupa chooni kichanga jinsi ya kiume na kusababisha kifo chake.

Mwenyekiti wa mtaa huo Juma Mbuza amesema walimtilia shaka mtuhumiwa Februari 18 mwaka huu katika klabu ya pombe za kienyeji baada ya kutoonekana na ujauzito,ndipo walipomuuliza kulikoni naye kudai kuwa amejifungua lakini mtoto yupo nyumbani.

Kauli hiyo haikumridhisha Mwenyekiti huyo ndipo alipoamua kumtafuta balozi wake aitwae Daud Dule na kumuuliza mtoto yupo wapi ndipo alipoanza kuwa na wasiwasi hali iliyowalazimu kumkamata kutoa taarifa kituo cha Polisi Iyunga ambapo kabla ya kufika Kituoni majira ya saa kumi na moja jioni mtuhumiwa alikiri kujifungua na kutupa kichanga chooni Februari 18 mwaka huu

No comments: