Huyu ni Baraka kijana mrefu kitanzania |
Inasemekana ni kijana mrefu kuliko wote Tanzania. Kijana huyu (katikati
pichani) ambaye anadhaniwa ni mrefu kuliko vijana wote Tanzania anaishi
maeneo ya Gongolamboto, Banana jijini Dar es salaam. Kijana huyu huwa
haonekani sana mitaani, lakini aliingia mjini siku hiyo na kuleta kizaa
zaa kikubwa pale alipoibuka mitaa ya Aggrey, Kariakoo. Alikuwa kivutio
kwa kila aliyemuona, alifunga mtaa watu wakimshangaa na kumgombania
kupiga nae picha. Kila aliyetaka kupiga nae picha alitoa Shilingi elfu
moja Tsh. 1000.
Picha hiyo amepigwa ndani ya Kinyozi (Salon) aliyoingia kupunguza nywele
zake na umati wa watu walikuwa nje ya kinyozi huyo kumsubiri atoke.
Mpaka sasa hajajulikana jina lake kamili na anafanya nini. Inasemekana
kuna watu wanamfuatilia kumsaidia umaarufu.
Hapa Hasheem Thabit alipokutana na Baraka |
JULIUS CHARLES |
UKIMUANGALIA kwa mara ya kwanza mchezaji wa Tanzania anayecheza
timu ya kikapu ya Oklahoma City Sounders inayoshiriki Ligi ya Kikapu
Marekani (NBA), Hasheem Thabit unaweza kujiridhisha kwamba ni mrefu
kuliko Watanzania wote uliowahi kuwaona. Ana futi 7.3.
Lakini mjini Bagamoyo katika Mkoa wa Pwani kwenye
shule ya Lord Barden yupo mchezaji anayemzidi Hasheem kwa urefu akiwa na
futi 7.5. Si mwingine namzungumzia Julius Charles (18) ni maarufu zaidi maeneo ya
Bagamoyo, na umaarufu huo umetokana na kimo chake huku wengi wakimuita
mpinzani wa Hasheem Thabit kutokana na urefu alionao ambao umepitiliza
na ukikutana naye lazima utishike au ubaki ukimshangaa
No comments:
Post a Comment