Zanzibar.
Watu wanne wamejeruhiwa baada ya milipuko minne inayoaminika kuwa ni
mabomu kutokea katika maeneo matatu tofauti Zanzibar.
Katika
moja ya matukio hayo, watu wanne walijeruhiwa, mmoja akikatika mguu,
katika eneo la Unguja Ukuu, Mkoa wa Kaskazini Unguja. Majeruhi wawili
wamelazwa katika Hospitali ya Mnazi Mmoja, Unguja.
Mkuu wa
Operesheni wa Polisi, Mkoa wa Kusini Unguja, Hamad Said Masoud alisema
mlipuko wa kwanza ulitokea juzi katika eneo la Fuaoni Maili Nne wakati
watu wasiojulikana waliporusha kitu kinachoaminika kuwa ni bomu wakati
waumini wa Kanisa la Evangelist wakiendelea na ibada ya Jumapili.
Kamishna
wa Polisi Zanzibar, Hamdan Omar Makame alisema tukio la juzi, kitu
kinachosadikiwa kuwa ni bomu kilirushwa wakati waumini wa kanisa hilo
wakiendelea na ibada na kutoa mlipuko na kishindo kikubwa. Alisema
wakati wakiendelea na uchunguzi wa tukio hilo, milipuko mingine mitatu
ilitokea jana.
Katika
mlipuko wa kwanza kwa jana uliotokea saa 6.30 mchana katika kituo kimoja
cha fundi vyuma aliyetambulika kwa jina la Juma Abdallah huko Unguja
Ukuu ndiko kulikokuwa na watu waliojeruhiwa.
Waliojeruhiwa katika tukio hilo ni Pandu Haji Pandu aliyekatika mguu na Shaaban Khamis Ibrahim ambaye aliumia sehemu za kiuno.
Hamad alisema mtu mmoja aliokota chuma kizito na kukipeleka kwa fundi akitaka atengenezewe nanga kwa ajili ya uvuvi.
No comments:
Post a Comment