Saturday 15 February 2014

Nape atofautiana na Jaji Warioba Bunge la Katiba

Katibu wa Itikadi na Uenezi wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Nape Nnauye (pichani), amesema Bunge Maalumu la Katiba, litatekeleza majukumu yake kwa kufuata Sheria ya Mabadiliko ya Katiba na si mawazo ya mtu yeyote.              
          Kauli hiyo ya Nape imekuja siku moja baada ya Mwenyekiti wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba, Jaji Joseph Warioba kusema kuwa litakuwa jambo lisilo la kawaida kwa Bunge hilo kubadili hoja ya msingi iliyopo kwenye Rasimu ya Katiba, akisisitiza kuwa jukumu lake ni kuifanyia marekebisho.
        Warioba alisema hayo juzi alipokuwa akizungumza katika mkutano ulioandaliwa na Kituo cha Demokrasia Tanzania (TCD), kuhusu tafakuri na maridhiano kuelekea katika Katiba Mpya.

No comments: