JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIASimu: 255 22 2460735/2460706
WIZARA YA UCHUKUZI
MAMLAKA YA HALI YA HEWA TANZANIA
FAKSI: 255 22 2460735/2460700
Barua pepe: met@meteo.go.tz
Tovuti: Tanzania Meteorological Agency - Admin -
S.L.P. 3056
DAR ES SALAAM
Unapojibu tafadhali nakili:
Kumb. Na.: TMA/1622
10 Februari, 2014
Taarifa kwa Umma: Matarajio ya kuwa naVipindi vya Mvua kubwa, Upepo Mkali na Mawimbi Makubwa.
Taarifa Na. 201402-01 Muda wa Kutolewa: Saa za Afrika Mashariki Saa 11 Jioni Daraja la Taarifa: Tahadhari Kuanzia: Tarehe 11 Februari, 2014 Mpaka: Tarehe 13 Februari, 2014 Aina ya Tukio Linalotarajiwa 1. Vipindi vya mvua kubwa (zaidi ya mm 50 ndani ya saa 24)
2. Hali ya Upepo mkali unaozidi kilomita 40 kwa saa
pamoja na mawimbi makubwa zaidi ya mita 2.0Kiwango cha uhakika: Wastani (60%) Maeneo yanayotarajiwa
kuathirika1. Vipindi vya Mvua Kubwa: Ukanda wa pwani mikoa ya Tanga,
Dar es Salaam, Pwani, Lindi, Mtwara pamoja na visiwa vya
Unguja na Pemba, Mbeya , Njombe, Ruvuma pamoja na kusini
mwa mkoa wa Morogoro
2. Upepo Mkali na Mawimbi Makubwa: Pwani ya mikoa ya Tanga,
Dar es Salaam, Pwani, Lindi, Mtwara pamoja na visiwa vya Unguja na PembaMaelezo:
Hali hii inatokana na kuwepo kwa kimbunga “FOBANE” kusini
magharibi mwa Bahari ya Hindi. Mfumo huu unatarajiwa kuvuta upepo kutoka Pwani ya Somalia na misitu ya Congo kuelekea maeneo ya nchi yetu.Angalizo:
Watumiaji wa bahari na wakazi wa maeneo hatarishi wanashauriwa kuchukua tahadhari. Maelezo ya Ziada
Mamlaka ya Hali ya Hewa inaendelea kufuatilia hali hii na itatoa
mrejeo pale itakapobidi
Imetolewa na
Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania.
Wednesday, 12 February 2014
HALI YA HEWA: Tahadhari kwa Umma
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment