Monday, 24 February 2014

ANAYEONA POSHO HAIMTOSHI AFUNGASHE VIRAGO’


bunge_4f64b.jpg
Dodoma. Wizara ya Fedha imepigilia msumari maombi ya wajumbe wa Bunge Maalumu la Katiba ya kutaka waongezewe posho na kusema anayeona ameacha kazi inayomlipa zaidi kwenda bungeni afungashe virago na kuondoka.
Msimamo huo umekuja siku moja tu baada ya gazeti hili kudokeza kuwa madai ya wajumbe wa bunge hilo kutaka waongezewe posho kutoka Sh300,000 za sasa kwa siku, yamegonga mwamba baada ya kamati iliyoteuliwa kuchunguza uhalali wake kusema kiwango hicho kinatosha.
Mwenyekiti wa muda wa bunge hilo, Pandu Kificho alisema jana bila kutaja viwango, kuwa ripoti ya kamati hiyo imewasilishwa kwa Rais Jakaya Kikwete kwa uamuzi.
Madai ya wajumbe kutaka waongezewe posho, yamechafua hali ya hewa ndani na nje ya Bunge, huku baadhi ya wananchi wakipaza sauti zao na kumsihi Rais Kikwete alivunje bunge hilo iwapo wajumbe watashikilia msimamo wa kutaka nyongeza ya posho

No comments: