Wednesday 19 February 2014

AC Milan vs Atletico Madrid

AC-Milan-vs-Atletico-Madrid


Kocha mpya wa AC Milan Clarence Seedorf amebeba taji la ligi ya mabingwa wa ulaya akiwa na vilabu vya AFC Ajax (1995), Real Madrid CF (1998) and Milan (2003, 2007) – ndio mchezaji pekee mwenye rekodi ya kubeba kombe hilo na timu zaidi ya mbili.
Diego Simeone kocha wa Atletico Madrid ana rekodi nzuri dhidi ya Seedorf, wakati walipokuwa bado wachezaji -Seedorf akiwa FC Internazionale Milano awalipoteza ubingwa wa Coppa Italia na Italian Super Cup finals dhidi ya timu aliyokuwa akiichezea Simeone SS Lazio mnamo mwaka 2000.
Milan wamepoteza mechi zao 4 zilizopita za hatua ya mtoano dhidi ya vilabu vya Hispania, dhidi ya Barcelona (2011/12 robo fainali, 2012/13 raundi ya 16 bora 16, 2005/06 nusu fainali) na dhidi ya RC Deportivo La Coruña (2003/04 robo fainali).

No comments: