Friday, 24 January 2014

Wenzetu wana barabara nzuri lakini ajali kama kawaida

Screen-Shot-2014-01-24-at-2.47.39-AM


Ajali imetokea huko Indiana Marekani… ni kwenye hizi barabara za kisasa ambazo nyingine zinaruhusu mpaka magari kuanzia manne kwenda mwelekeo mmoja lakini ikitokea mmoja akahama njia ghafla au akapinduka, madhara yanakua makubwa manake mara nyingi kuna wengine nyumba yake wako mbio. kwenye mwelekeo huohuo.
Unaambiwa mbali na magari madogo, idadi ya malori yaliyopata ajali kwenye hili tukio kwa pamoja yanafikia kumi na tano ambapo japo chanzo kamili hakijatolewa na Polisi, mmoja wa madereva anasema hali ya hewa ya weupe kutanda imechangia manake kama yeye mwanzoni aliona magari mawili tu mbele yake lakini kusogea karibu akakutana na mrundiko.
Imeripotiwa watu watatu ndio wamefariki huku wengine wanaokadiriwa kuwa zaidi ya 10 wakiwa wamejeruhiwa.
Screen-Shot-2014-01-24-at-2.47.14-AM
Screen-Shot-2014-01-24-at-2.47.25-AM
Screen-Shot-2014-01-24-at-2.50.36-AM

No comments: