Tuesday, 14 January 2014

CHRISTIANO RONALDO NDIYE MCHEZAJI BORA WA SOKA WA FIFA KWA MWAKA 2013

Cristiano1-Ronaldo-2013

Baada ya kuikosa tuzo ya Mchezaji Bora wa mwaka kwa zaidi ya mara 4, hatimaye mshambuliaji wa timu ya soka ya Real Madrid na Ureno, Christiano Ronaldo, muda mchache uliopita ametangazwa kuwa Mchezaji Bora wa Mwaka 2013 [FIFA World Player Of The Year] na France Football’s Ballon d’Or ambalo ni jarida la nchini Ufaransa linaloheshimiwa sana katika masuala ya soka. Utoaji wa tuzo hizo umemalizika muda mfupi kutokea Zurich nchini Switzerland yalipo pia makao makuu ya Shirikisho hilo la vyama vya soka ulimwenguni[FIFA]
Ronaldo 
 Ronaldo akiwa ameshikilia tuzo yake.
Katika tuzo hizo Ronaldo ambaye mashabiki wake wengi hupenda kumuita CR7 (kwa maana ya majina yake na namba ya jezi yake] alikuwa akichuana na wachezaji Lionel Messi [Barcelona na Argentina] na Frank Riberry[ Ufaransa na Bayern Munich]
Mara tu baada ya kutangazwa jina lake, Ronaldo ambaye alipanda jukwaani kupokea tuzo akiwa ameongozana na mwanae mdogo wa kiume [Christiano Ronaldo Jr], alishindwa kujizuia na kuonyesha furaha yake kwa machozi ya furaha. Jina la mshindi wa tuzo ya mwaka huu lilitangazwa na Pele wa Brazil [Mfalme wa Soka]
Katika mwaka 2013 Ronaldo alitikisa nyavu mara 66 kwa timu yake ya Real Madrid na nchi yake Ureno. Kura za kumchagua mchezaji bora wa FIFA hupigwa na manahodha wa timu za nchi zilizo chini ya FIFA, makocha na waandishi wa habari wanaoteuliwa kutoka katika nchi 209 zilizo wanachama wa FIFA.
Wakati huo huo kikosi cha dunia cha soka kimetangazwa na kuwa ni; Manuel Neuer (Bayern Munich, Germany); Dani Alves (Barcelona, Brazil), Sergio Ramos (Real Madrid, Spain), Thiago Silva (Paris Saint-Germain, Brazil), Philipp Lahm (Bayern, Germany); Andres Iniesta (Barcelona, Spain), Xavi Hernandez (Barcelona, Spain), Ribery (Bayern, France); Ronaldo (Madrid, Portugal), Zlatan Ibrahimovic (PSG, Sweden), and Messi (Barcelona, Argentina).

No comments: