Mwenyekiti
wa Umoja wa Makatibu wa Bunge wa Nchi wanachama wa Jumuiya ya Madola
barani Afrika na Katibu wa Bunge la Ghana Bwana Emmanuel Anyimadu
(kushoto) akifungua rasmi Mkutano wa Kamati ya Utendaji ya Umoja huo
jijini Dar es Salaam leo. Kulia ni Katibu Mkuu wa Umoja wa Makatibu wa
Bunge wa Nchi za Jumuiya ya Madola (Afrika), mwenyeji wa Mkutano huo na
Katibu wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Thomas
Kashililah. Makatibu
wa Bunge wa Nchi za Jumuiya ya Madola (Afrika) wakiwa kwenye Mkutano
wa kamati ya Utendaji Jijini Dar es Salaam. Washiriki katika Kamati ya
Utendaji wanatoka katika nchi za Ghana, Uganda, Tanzania, Botswana,
Kenya, Afrika Kusini na Zanzibar.
Picha ya pamoja ya Makatibu wa Bunge wa Nchi za Jumuiya ya Madola (Afrika) pamoja na maafisa waandamizi wakati wa Mkutano wa Kamati ya Utendaji Jijini Dar es Salaam. Lengo la Mkutano huu ni kuandaa Mkutano Mkuu wa Umoja wa Makatibu wa Bunge wa Jumuiya ya Madola (Afrika) utakaofanyika nchini Kenya mwezi Juni, 2014. (Picha na Prosper Minja – Bunge

No comments:
Post a Comment