Thursday, 16 January 2014

Unaambiwa Wachina wameanza kutengeneza upya Meli ya Titanic.

 
titanics

Nchi ya China ni Nchi inayoonekana kuwa na Wakazi wanaopendela ujenzi wa majengo makubwa ya kihistoria na magari kadhaa yenye muonekano wa alama ya uchina kama ishara ya kuonyesha ufanisi wao katika uvumbuzi wa vitu mbalimbali hapa duniani.
Kwa sasa China tunaweza kuwazungumzia kivingine katika jamii yetu  kwani mara kwa mara wameonekana ni watu wanaofanya vitu vikubwa sana na kwa sasa wachina wameamua kutengeneza meli kubwa kwa mfano wa meli maarufu ya Titanic.

china-titanic-replica-6d-tragedy-simulator-1-690x494

Kwenye kumbukumbu Meli ya Titanic iliyozama mwaka 1914 karibu karne moja iliyopita na kuua watu waliokadiriwa kuwa karibu elfu moja,sasa kampuni kutoka uchina ya Star Investment Group katika mkoa wa Sichuan imesema itatumia dola za kimarekani milioni 165 katika kuijenga upya mpaka kuikamilisha meli hiyo yenye mfano wa Titanic.

china-titanic-replica-6d-tragedy-simulator-3

Meli hiyo mpya ya wachina ambayo itafanana kabisa na meli ya Titanic iliyozama kwenye kina cha bahari karne moja iliyopita,Meli hiyo itajengwa kwa ushirikiano na kampuni ya serikali ya China Ship Building Corporation ya Wuchang inatumika kama sehemu ya hifadhi ya makumbusho katika mkoa wa Sichuan.
Katika meli hii ya Replica ni ishara ya uvumbuzi uliopita kikomo kutoka kwa wachina na wanategemea kuingiza mamilioni ya fedha kama riba kutokana na alama ya Titanic duniani

No comments: