Saturday, 25 January 2014

WATU WAWILI WAFARIKI DUNIA MKOANI IRINGA KWA MATUKIO TOFAUTI


Rpc - Mungi 
Watu wawili wafariki dunia mkoani Iringa katika matukio mawili tofauti likiwemo la Thobias Godlove (26) mkazi wa Mbeya kugongana uso kwa uso na fuso  maeneo ya Maguvani katika barabara ya Iringa – Mbeya wilaya ya Mufindi.
 
Mwandishi wa matukiodaima.com  Diana Bisangao anaripoti  kutoka Iringa kuwa , Kamanda wa polisi mkoani Iringa Ramadhani Mungi alithibitisha kutokea kwa tukio hilo lililotokea mnamo tarehe 23 januari majira ya saa 12 kamili alfajiri.
 
Kamanda Mungi alisema marehemu alikuwa akiendesha gari aina ya Toyota Noah lenye namba za usajili T 828 BTR akiwa amepakia abiria sita aligongana na gari aina ya Mitsubishi Fuso lenye namba za usajili T 537 BGX mali ya Fred Benedict lililokuwa likiendeshwa na Emilik Kibiti (42) mkazi wa Makambako.
 
Hivyo majeruhi sita walikimbizwa katika Hospitali ya Ilembula na dereva wa fuso alikamatwa kwa mahojiano Zaidi huku chanzo cha ajali hiyo ni mwendo kasi kwa madereva.
 
Na katika tukio lingine mkazi wa Ilula Sokoni kata ya Nyalumbu tarafa ya Mazombe wilaya ya Kilolo Bwana Kamongo Kikoti (38) alikutwa amefariki dunia baada ya kujinyonga juu ya mti kwa kutumia kamba ya katani.
 
Kamanda Mungi alithibitisha kutokea kwa tukio hilo lilitokea mnamo tarehe 23 januari majira ya saa 11:20 jioni huku chanzo cha kifo hicho ni marehemu alikuwa na matatizo ya akili.
 

No comments: