Tuesday, 21 January 2014

WATU 9 WAFARIKI DUNIA NA 30 KUJERUHIWA KATIKA AJALI MKOANI LINDI LEO


BASI Likiwa limeanguka na maiti bado zilikuwa hazijatolewa chini
Kamishna msaidizi wa Jeshi la Polisi mkoa wa Lindi,Renatha Mzinga akisimamia zoezi la kuinua basi hilo kwa ajili ya utoaji wa Maiti  9 za ajali hiyo.



 Baadhi ya abiria ambao walikuwemo katika basi hilo wakiwa wametoka bila kujeruhiwa

Watu 9 wakiwemo watoto 2 wamefariki dunia na wengine zaidi ya 30 kujeruhiwa vibaya baada ya basi la abiria la Alhamdulilah linalofanya safari zake kutoka jijini Dar kwenda mkoani Mtwara kupinduka katika kijiji cha Mambulu Manispaa ya Lindi. 
 Ajali hiyo iliyotokea mchana leo baada ya basi hilo kupishana na lori na kupoteza mwelekeo na kupinduka hali ilichangiwa na mvua iliyokuwa ikiendelea kunyesha.
 Hadi ninatoka eneo la tukio marehemu hao hawakuweza kufahamika kwa haraka kutokana na kukatika viungo na tayari majeruhi na maiti wote wamefikishwa hospitali.
Kamanda wa polisi wa mkoa wa Lindi,George Mwakajinga ambae alikuwepo katika eneo la ajali hiyo hakuweza kuongea lolote kutokana na kutingwa na harakati za kuokoa majeruhi wa Ajali hiyo Taarifa zaidi za majeruhi hao pamoja na maiti zilizotambuliwa tutawajuza

No comments: