Unaambiwa Tanzania kuna vijiji elfu kumi na tisa na mia mbili kwa mujibu wa sensa ya Mwaka 2012 iliyohusisha makazi na watu ambayo pia ilionyesha Watanzania ni milioni 44.9
Sasa basi, katika hivyo vijiji 19,200 kuna vijiji zaidi ya mia mbili ambavyo mpaka sasa vina tatizo kubwa la mawasiliano, yani ukiwa na simu ya mkononi ni noma… hauwezi kuwasiliana kirahisi sababu hakuna mawasiliano ya uhakika, ni kubahatisha pengine mpaka usimame sehemu flani.
Vijiji ambavyo havina mawasiliano ya simu mpaka sasa ni zaidi mia mbili hilo likiwa ni tatizo sugu.
Idadi ya kupunguza vijiji vyenye tatizo la mawasiliano haijaanza kupunguzwa leo na TCRA (mamlaka ya mawasiliano) kwani kwa miaka mitano iliyopita ilifanyika kazi ya kuvipa mawasiliano ya uhakika vijiji zaidi ya mia moja.
Kwa sasa Serikali inaendelea kuvisaidia hivi vilivyobaki baada ya kupokea msaada wa shilingi bilioni 17.5 kutoka benki ya dunia ambazo zitatumika kujenga minara kwenye vijiji 869 vyenye jumla ya wakazi milioni 1.6.
No comments:
Post a Comment