Wednesday, 29 January 2014
Monday, 27 January 2014
SERIKALI YAPUNGUZA GHARAMA ZA KUUNGANISHA UMEME
Prof. Sospeter Muhongo
*Ni kwa wanavijiji wanaoishi jirani na bomba la gesi Mtwara - Dar
SERIKALI imeamua kupunguza
kwa kiasi kikubwa bei ya kuunganisha umeme majumbani na kufikia sh.
27,000/ kwa wanavijiji wanaoishi kwenye maeneo ambayo bomba la gesi
linapita.
“Jana Waziri
Mkuu aliagiza tutafute namna ya kuwasaidia wananchi wanaoishi jirani na
njia ya bomba la gesi. Nami nilikaa na wasaidizi wangu jana usiku na
kufanya hesabu na tukaamua tuweke kiwango hicho kwa ajili ya wakazi
hao,” alisema.
Alisema katika mikoa mikoa mingine gharama za
kuunganisha umeme ni sh. 177,000/- lakini kwa mikoa ya Lindi na Mtwara
gharama hizo zilishushwa na kufikia sh.99,000/-. “Lakini sasa hawa
wenzetu tumewapa upendeleo zaidi na tumewapunguzia gharama hizo hadi sh.
27,000/-,” alisema huku akishangiliwa.
Gharama hizo ni maalum kwa ajili ya wakazi waishio
jirani na bomba hilo linaloanzia Mtwara hadi Dar es Salaam kupitia mikoa
ya Lindi na Pwani.
Choo cha Birdman kilichotengenezwa na dhahabu, kichokadiliwa kuwa na thamani ya $1mil hiki hapa.
Birdman boss wa record label ya YMCMB ambaye mara nyingi huwa anajisifia kwa matumizi yake makubwa ya pesa kwenye vitu luxury, ameendeleza hivyo vitendo vya kufanya matumizi makubwa ya pesa.
Hivi karibuni ame-share picha ya choo chake ambacho kime-kuwa covered na material ya dhahabu pande zote.
Mfuniko wake na sehemu ya juu ya choo hicho ni dhahabu tupu na sehemu nyingine yote hautaweza kukiona hicho choo kwasababu kimefunikwa na dhahabu.
Gharama yake inakadiliwa na kuwa na thamani ya dola millioni moja.
Sunday, 26 January 2014
BREAKING NEWSSSS MKUU WA POLISI WILAYA (OCD) IRINGA APATA AJALI
wasomi wa chuo kikuu cha Iringa wakitazama ajali hiyo ambayo dereva wake OCD Iringa alinusurika kifo na kuumia mkono wake kiasi |
ABANIKWA KAMA KUKU, NI BAADA YA KUTUHUMIWA KUIBA BODABODA MAFINGA
Ezekiel Kaganga |
Kamanda
wa Polisi Mkoa wa Iringa, Ramadhani Mungi amewataja watu wawili wakihusishwa na
tukio hilo la kinyama.
Aliwataja
waliokamatwa kuwa ni ni Alex Ludago (28) na Steven Michael (29) wote wakazi wa
MET mjini Mafinga.
Akisimulia
jinsi tukio lilivyokuwa katika wodi namba tano ambako amelazwa Kaganga alisema
anafahamiana na watuhumiwa hao na kabla ya tukio hilo Januari 7, mwaka huu walikuwa
pamoja wakinywa bia katika moja ya maduka ya kuuzia pombe mjini Mafinga.
Alisema
Januari 8 mwaka huu alipokea taarifa katika duka hilo la pombe lililopo katika eneo
la mashine ya mpunga kwamba kuna pikipiki ilipotea katika mazingira ya
kutatanisha baada ya yeye kuondoka katika eneo hilo siku iliyopita.
Katika
majibu yake kwa mmoja wa watuhumiwa hao alisema hajui lolote kuhusu kupotea kwa
pikipiki hiyo.
Anavyoonekana majereha ya mgongoni |
“Jamaa
hao hawakuridhishwa na majibu yangu na Ijumaa ya Januari 12 alikamatwa na Polisi akihusishwa
na tukio hilo na akatoka Januari 17,” alisema.
Alisema
baada ya kutoka Polisi alikaa siku tatu uraiani na ndipo alipokamatwa na vijana
hao na kupelekwa katika msitu wa Lumwago nje kidogo ya mji wa Mafinga.
Katika
msitu huo alifungwa kamba, kupigwa viboko na baadaye alining’inizwa juu ya mti
huku moto ukiwa umechomwa chini yake.
Sehemu ya miguu yake |
“Nilibanikwa
kama kuku, moto ukiwa chini mie nikiwa nimefungwa juu ya miti; niliachwa hapo
kwa siku mbili,” alisema.
Alisema
baada ya siku mbili alihamishwa kutoka katika msitu huo na kupelekwa eneo la
machijio mapya na kumwagiwa mafuta ya taa ili achomwe na moto na kundi la watu
wanaokadiriwa kuwa saba.
“Nikiwa
mahututi walinichukua na kunipeleka kituo cha Polisi kabla sijaletwa hapa
hospitalini nako endelea kupata matibabu,” alisema.
Aliyata
maeneo ambayo ameungua sana kuwa ni mgongoni, makalioni, mikononi, ubavuni,
miguuni na shingoni.
Kaka
wa Kaganga, Aizaki Kaganga alisema “mdogo wangu anaendelea kupata matibabu, na
hali yake sio mbaya sana japokuwa hawezi kutembea.”
Alisema
alipokea taarifa ya kupotea kwa mdogo wake
kuhusishwa na tukio hilo na akawaahidi watuhumiwa wamsubiri arudi kutoka safarini Arusha ili alipe
pikipiki hiyo.
“Hata
hivyo vijana hao hawakuwa na subira hiyo na badala yake wakamfanyia unyama
waliofanya,” alisema.
Kamanda
Mungi alisema jeshi la Polisi linaendelea na uchunguzi wa tukio hilo pamoja na
kuwasaka watuhumiwa wengine waliohusika na tukio hilo.
Akifarijiwa na kaka yake |
Subscribe to:
Posts (Atom)