Thursday, 11 December 2014

Unajua nini alichoamua mpenzi wa Ray J baada ya mahusiano yao kuvunjika? Stori iko hapa

gunnnnnn

Mkali wa muziki  wa RnB na Hip Hop nchini Marekani William Ray maarufu kama Ray J ameamua kuachana na mpenzi wake Princess lakini kitendo hicho kilimkasirisha mwanadada huyo na kuamua kutaka kujiua.
Kwa mujibu wa Taarifa iliyotolewa inasema Ray J aliamua kuachana na rafiki yake huyo wa kike usiku wa jumanne lakini hawakufikia maamuzi hali iliyomfanya msichana huyo kutamka kutaka kujiua.
Licha ya kutotoa sababu za msingi za kuachana kwao siku ya jana Ray J na mpenzi wake waliishia kutoelewana na kuzusha ugomvi mkubwa kati yao.
ray

Anasema aliamua kuwataarifu Polisi kwani ndani kwake kulikua na bastola ambayo angeweza kuitumia kujiua kama alivyofanya rafiki yao Stephanie Moseley.
Baada ya kupatiwa taarifa hiyo wana usalama walikwenda nyumbani kwa mwanamuziki huyo lakini hawakumkuta msichana huyo na walipozungumza na Ray J aliwaambia amezungumza naye na kusisitiza hatafanya kitendo hicho tena.
Ray J pia alishawahi kuwa na uhusiano na mwanamitindo Kim Kardashian mwaka 2006

No comments: