Bondia Floyd Mayweather ametaja tarehe 2 mwezi May mwaka 2015 kama siku ya pigano kati yake na Manny Pacquiao .
Kulingana
na gazeti la Daily mail nchini Uingereza ,uvumi kwamba pigano hilo
ambalo litakuwa la kiwango kikubwa cha malipo kuwahi kutokea katika
historia ya ndondi ulianza pale Pacquiao alipoonyesha mchezo mzuri kati
yake na Chris Algieri mjini Macau wiki mbili zilizopita.
Na sasa
Maywheather kupitia kampuni yake moja ya mauzo amesema kuwa yuko tayari
kupambana na Pacman katika pigano lake linalokuja.
Bondia huyo ambaye ndiye
mwanamichezo tajiri duniani amesema kuwa mashabiki wa ndondi wamesubiri
sana pigano hilo na sasa yuko tayari.
''Kizuizi kikubwa cha pigano
hilo ni promota wa Pacquiao Bob Arum ,lakini najua kwamba sisi sote
tunalihitaji pigano hili'',alisema Mayweather.. Kwa hivyo ni wakati
lifanyike.
Mayweather alikiri kwa mara ya kwanza majadiliano
yanaendelea kwa siri na kuongeza kwamba hamuogopi mtu yeyote.''Miaka
iliopita tulikuwa na tatizo la kupimwa mikojo na damu,swala ambalo
Pacman amekuwa akilipinga''.aliongezea Mayweather.
Hatahivyo upande wa Mayweather ni vile kitita cha pigano hilo kitakavyogawanywa.
Inakadiriwa kuwa pigano hilo litagharimu dola millioni 300.
Upande
wa Pacman tayari umekubali fedha hizo kugawanywa kwa 60-40 huku
Mayweather akichukua kitita kikubwa,ijapokuwa kuna madai kwamba
Mayweather huenda akadai asilimia kubwa zaidi iwapo makubaliano
yataafikiwa
No comments:
Post a Comment