Unamkumbuka yule mfanyakazi wa ndani
aliyemtesa mtoto nchini Uganda na kuteka hisia za watu wengi duniani?
leo kesi yake imeweza kusomwa kwa mara nyingine.
Mfanyakazi huyo Jolly Tumuhirwe
mwenye miaka 22 aliiambia mahakama nchini humo leo kuwa anajua kile
alichokifanya na anakiri kosa hivyo anaomba watu wamsamehe kwa kuwa
alifanya makosa.
Mfanyakazi huyo wa nyumbani
aliyenaswa kwenye kanda ya video akimpiga mtoto wa bosi wake ajulikanaye
kwa jina la Arnella mwenye umri wa miezi 18 pia alikua akimkanyaga
mtoto huyo bila huruma.
Licha ya taarifa ya polisi kusema Jolly atashitakiwa kwa kosa la
jaribio la mauaji, kiongozi wa mashitaka alimshitaki kwa kosa la kumtesa
mtoto mdogo.Msichana huyo alikiri makosa yake na kuomba msamaha na Hakuna wakili yeyote aliyemwakilisha Jolly mahakamani hapo licha ya mmoja wa mawakili mashuhuri kusema angemwakilisha Jolly bila malipo ypyote.
Kesi hiyo imeahirishwa tena hadi keshokutwa wakati hakimu akitarajiwa kutoa hukumu dhidi yake.
Binti huyo huenda akafungwa jela miaka 15 au kutozwa faini ya dola za kimarekani 800 au adhabu zote mbili.
No comments:
Post a Comment