Tuesday, 9 December 2014

Mtoto wa Malkia wa Uingereza kwa mara ya kwanza ndani ya ‘White House’ ya Marekani

white

Familia ya Kifalme ya Prince Willium na mkewe Kate Middleton wako nchini Marekani katika ziara yao ya kwanza ambapo watakua kwa muda wa siku tatu.
prince

Mtoto huyo wa malkia wa Uingereza  Prince Willium na mkewe wako katika ziara hiyo na jana alipata nafasi ya kufanya mazungumzo na Rais wa nchini hiyo Barack Obama ndani ya ikulu hiyo kwa mara ya kwanza.
toto

Wakati akifanya mazungumzo na Rais huyo kwa upande wa mkewe Kate Middleton ambaye  ni mjamzito wa miezi mitano aliweza kutembelea kituo cha maendeleo cha watoto kilichopo katika mji wa Newyork na kufanya nao mazungumzo ambapo aliongozana na Meya wa jiji hilo Chirlane McCray.
Mbali na hayo pia familia hiyo ya malkia wa Uingereza Elizabeth,pia ilipata nafasi ya kutazama tamaduni mbalimbali za nchi hiyo na kupata muda wa kwenda kuangalia mchezo wa mpira wa mikono kati ya Brooklyn Nets dhidi ya Cleveland Cavaliers ambapo walikuatana na mastaa wa muziki Beyonce pamoja na mumewe Jay-z  wakiangalia mchezo huo.
bey

No comments: