Naibu
Kocha wa Kilabu ya Aston Villa Roy Keane na mshambuliaji Gabriel
Agbonlahor nusra wapigane wakati wa mazoezi katika majibizano ya manane
yaliomlazimu kocha huyo kuondoka katika kilabu hiyo.
Kulingana na
gazeti la Daily mail nchini Uingereza,Roy Keane mara kwa mara alihusika
katika mgogoro na wachezaji wa muhimu wa kilabu hiyo miezi sita tu baada
ya kujiunga na kilabu hiyo.
Inadaiwa kuwa hali ya mazingira wakati wa mazoezi ilibadilika mara kwa mara wakati wa kuwasili kwa Roy Keane.
Kulikuwa
na hali ya wasiwasi wakati kocha huyo alipozozana na nahodha wa kilabu
hiyo Agbonlahor mbele ya wachezaji wenzake wakati wa mazoezi kabla ya
naibu huyo kuondoka katika timu hiyo.
Inadaiwa kuwa Agbonlahor alikuwa akijadiliana na mkufunzi wa timu hiyo Lambert wakati Keane alipoingilia kati.
Lakini Agbonlahor alikataa kunyamaza na badala yake akamwambia Keane kwamba anazungumza na kocha.
Wawili hao baadaye walihusika katika majibizano na ilibidi watawanywe.
Uhasama
huo uliendelea kati ya wawili hao ndiposa Lambert akafanya kikao na Roy
Keane wakati ilipoamuliwa kwamba nahodha huyo wa kitambo wa timu ya
Manchester United ataondoka katika kilabu hiyo
No comments:
Post a Comment