Monday 8 December 2014

Korti yatupilia mbali kesi ya 'fungate'

                      
                 Dewani ndiye alikuwa mshukiwa mkuu wa mauaji ya mke wake
Mahakama nchini Afrika Kusini imetupilia mbali kesi dhidi ya Shrien Dewani , mfanyabiashara mwingereza anayetuhumiwa kuwakodi mamluki waliomuua mkewe Anni Dewani wakati wa fungate yao mjini Cape Town.
Jaji Jeanette Traverso alimuondolea mashitaka bwana Dewani akisema upande wa mashitaka, ulikosa kutoa ushahidi wa kutosha kuwezesha kesi hio kuendelea.
Pia alisema ingekuwa vigumu sana kwa Bwana Dewani kupatwa na hatia kwani kesi ilivyokua inaendeshwa ingebidi bwana Dewani kukiri kuwa alihusika na mauaji , kitu ambacho kwa kweli hakingeweza kufanyika.
Pia alipuuza ushahidi wa shahidi mkuu wa upande wa mashitaka aliyekua dereva wa Taxi, ambaye kwa sasa anatumikia kifungo kwa mauaji hayo pamoja na watuhumiwa wenzake.
Jaji alisema ushahidi wao ulikuwa na makosa mengi na uongo.
Dadake Ani, Ami Denborg aliangua kilio baada ya jaji kutoa hukumu yake akikosoa mfumo wa sheria wa Afrika Kusini.
Akiongea nje ya mahakama mamlaka ya uongozi wa mashitaka ilisema kuwa ''ni jambo la kusikitisha kwamba Dewani amefutiwa mashitaka kwa sababu tunaamini kuwa alihusika. ''
Aliongeza kuwa ''mahakama haijaonyesha kuwa hana hatia, bali imesema eti haiamini ushahidi wa mashahidi watatu waliohusishwa na kesi hio ambao wenyewe walifungwa jela kwa mauaji hayo

No comments: