Mkutano wa Umoja wa Mataifa kuhusu
mazingira ambao ulikuwa umalizike mapema, unaendelea nchini Peru kwa
siku ya 13 huku wajumbe wakijaribu kufikia makubaliano kuhusu namna ya
kupambana na kuzidi kwa joto duniani.
Wamekwama katika hoja kuhusu ahadi ambazo zinaweza kutolewa na nchi zilizoendelea na zinazoendelea.
Mataifa
yanayoharibu mazingira zaidi, kama Marekani na ya Umoja wa Ulaya,
yanataka kutangaza mwaka ujao yatapunguza gesi inayozidisha joto kwa
kiasi gani.
Lakini piya yanataka nchi nyengine zaidi zitoe ahadi kama hiyo.
Nchi
kuu zinazoendelea, pamoja na India na Uchina, zinapinga hayo huku nchi
maskini zaidi zinataka msaada zaidi wa fedha ili kupambana na athari za
mabadiliko ya hali ya hewa.
No comments:
Post a Comment