Monday 8 December 2014

Kampuni ya Taxi nchini India matatani

 
Serikali ya India imepiga marufuku huduma za kampuni ya kimataifa ya magari ya kukodisha,Uber baada ya dereva wake mmoja kushutumiwa kumbaka abiria wa kike.
Afisa wa idara ya usafirishaji amesema Kampuni hiyo imeorodheshwa kwa kuwapotosha wateja.
Mwanamke mmoja 26, alitumia simu ya mkononi kuomba kupata huduma ya Taxi kuelekea nyumbani siku ya ijumaa badala yake alipelekwa mafichoni na kubakwa.
Dereva ambaye alikamatwasiku ya jumapili akihusishwa na kitendo hicho amefikishwa mahakamani.
Kampuni ya Uber iliyojipatia umaarufu nchini India, imeshutumiwa kushindwa kuwachunguza kwa ukaribu madereva wake.
Idara ya usafirishaji imepiga marufuku shughuli zote zinazohusiana na kutoa huduma ya usafirishaji kupitiawww.Uber.com, Shirika la habari la ufaransa, AFP limeeleza.
Maafisa wamesema Uber, huenda ikapigwa faini au kufungiwa kabisa kufanya kazi zake.

No comments: