Saturday 13 December 2014

Matokeo ya Simba vs Yanga

Screen Shot 2014-12-13 at 7.09.29 PM
Timu ya Simba imeibuka na ushindi baada ya kuichapa timu ya Yanga 2-0 huku timu ya Yanga wakiambulia kuondoka na maumivu ya kushindwa kufurukuta kwa bao hata moja.
Wafungaji wa magoli kutoka timu ya Simba ni Awadh Juma na Elias Maguri ambapo mabao yote yamefungwa katika kipindi cha kwanza.
Kwa mara ya pili tena timu ya SIMBA wamefanikiwa kuibuka na ushindi wa Nani Mtani Jembe baada ya kutwaa ubingwa huo mwaka jana walipoichapa Yanga bao 3 -1.
Kwa upande wa zawadi Simba wamefanikiwa kutwaa milioni 92 huku Yanga wakiondoka milioni 7.
 Wachezaji wa timu ya Simba wakishangilia bao la pili lililofungwa na Elias Maguli katika dakika ya 40 ya kipindi cha kwanza. Mabao yote ya Simba yamefungwa katika kipindi cha kwanza huku bao la kwanza likifungwa na Awadh Juma katika dakika ya 30.
 Mashabiki wa Simba wakishangilia moja ya mabao yaliyofungwa na timu yao.
 Andreu Coutihno, akimiliki mpira katikati ya mabeki wa Simba…
Mchezaji mpya wa Yanga, kutoka nchini Liberia, Kpah Sherman. akisomba kijiji cha mabeki wa Simba…. Hadi mpira unaisha jumla ya mashabiki wasiopungua wanne wa Yanga walikuwa wameshazimia uwanjani. 
Mashabiki wa Simba waliojaza kwenye dimba la uwanja wa taifa

Umati wa wana jangwani leo taifa

No comments: