Baraza
la wazee wa Klabu ya Yanga, leo limetoa tamko la kusitisha maandamano
yao ambayo walikuwa wameyapanga kufanyika ili kushinikiza serikali kutoa
kibali cha Ujenzi wa uwanja wao wa kisasa unaotarajia kujengwa sehemu
ya Jangwani, Dar es Salaam.
Tamko
hilo la kusitisha maandamano hayo limetoleo mara baada ya baadhi ya
viongozi wa juu wa timu hiyo kukutana na viongozi wa serikali.
Viongozi
hao wa serikali walitoa tamko kuhusu kushughulikia ombi lao hali
iliyosababisha viongozi wa Yanga kusitisha maandamano yao waliyokuwa
wameyapanga kuyafanya juma hili.
Juma lililopita Katibu wa baraza hilo, Ibrahim Akilimali alitoa siku tano kwa Baraza la Madiwani Manispaa ya Ilala, liwe limewapa kibali cha ujenzi huo, vinginevyo waliahidi kufanya maandamano makubwa.
Amesema viongozi wa juu wa klabu hiyo walikutana na viongozi wa serikali akiwemo Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Sadik Mecky Sadik, Meya wa Ilala Jery Silaa na Diwani wa Kata ya Jangwani ambapo walikubaliana ombi lao kufanyiwa kazi.
Akilimali
amesema serikali kupitia Manispaa ya Ilala ilieleza kuwa ombi lao
linashughulikiwa kwa haraka, hivyo aliwataka wanachama wa klabu hiyo
kuelewa jambo hilo bila kuwepo na migogoro.
Ameweka wazi kuwa wanaamini serikali kupitia Manspaa ya Ilala watalishughulikia ombi lao, ingawa amesisitiza kuwa ikitokea ombi lao hilo linaloshughulikiwa likija na majibu ya “hapana” watatafuta mbinu nyingine.
"Sisi tumeomba hivyo majibu ni mawili ndiyo tumepata au tumekosa, ikitokea likaja jibu la kukosa hapo ndiyo kutakuwa na utata na kuamua cha kufanya," alisema katibu huyo wa baraza la wazee wa klabu ya Yanga.

Ameongezea
kuwa klabu hiyo imejiandaa kuwalipa watu waliongezeka katika eneo lao,
hivyo hawaoni sababu za kwenda kujenga nje ya mji wakati wao ni watoto
wa mjini.
No comments:
Post a Comment